 |
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani, Pereira Ame Silima (kushoto)akipokea sehemu ya ya stika maalum
kwa ajili ya kampeni ya usalama barabarani toka kwa wadhamini wa stika
hizo kwa mwaka huu Airtel na Puma, wanaokabidhi (kutoka kulia) ni
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano na Mkurugenzi
wa kampuni ya Mafuta Puma Bw. Maregesi Manyama. Anayeshuhudia ni
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga. Airtel
Tanzania na Puma ni wadhamini wakuu wa wiki ya uhamasisaji wa wiki ya
Nenda kwa usalama ambapo mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani Iringa
ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa
vitendo, zingatia sheria. |
 |
Kamanda Mpinga akionyesha jinsi ya kufungua na kubandika stika hizo maaalum.
Kamanda
wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga akipokea msaada
wa fulana 1000 za kuhamasisha wiki ya usalama barabarani na vipeperushi
500 kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL), Teddy Mpunda katika makabidhiano yaliyofanyika kwenye
makao makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dar es salaam.
Kushoto ni Meneja wa Mipango Endelevu na Uwajibikaji kampuni ya
Serengeti, Nandi Mwiyombela. Vifaa hivyo vina thamani ya shilingi
milioni 17.5 na kampuni hiyo imesema inaangalia uwezekano wa kuchapisha
vipeperushi vingine kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam ambapo hivi vya
awali vitapelekwa mikoani. | | | | | | | | | | | |
on Saturday, September 15, 2012
Post a Comment