Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein
amefanya uteuzi wa Manaibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha
Zanzibar(SUZA).
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa
na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Zanzibar DKT.
Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa DKT Shein amemteuwa DKT.Zakia
Mohammed Abubakar kuwa Naibu Makamo Mkuu wa SUZA ataeshughulikia masuala
ya Utawala.
Pia DKT Shein amemteuwa DKT Haji Mwevura kuwa Naibu Makamo Mkuu wa Chuo hicho atakaeshughulikia masuala ya Taaluma.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein
amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya
kifungu10(1)cha Sheria ya SUZA namba 8 ya mwaka 1999 kama
ilivyorekebishwa na kifungu cha 4 cha Sheria namba 11 ya mwaka 2009.
Uteuzi huo umeanza leo.
Post a Comment