Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT
Ruvu na Simba iliyochezwa jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 73,611,000.
Washabiki 12,884 walikata tiketi
kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000,
sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 16,154,161.02 wakati
asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh.
11,228,796.61.
Mgawo mwingine umekwenda kwa
msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 150,000,
waamuzi sh. 70,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, tiketi sh. 3,175,000,
maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium
technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 300,000, ulinzi na
usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 5,384,720.34, Mfuko wa
Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 3,230,832.20, uwanja sh.
5,384,720.34, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh.
1,076,944.07, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
1,076,944.07.
61 WASHUHUDIA MECHI YA AFRICAN LYON v POLISI MORO
Watazamaji 61 ndiyo waliokata
tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya African Lyon na
Polisi Moro iliyofanyika jana (Septemba 19 mwaka huu) Uwanja wa Azam
Complex, Dar es Salaam.
Mapato yaliyopatikana katika
mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 5,000 ni sh.
185,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 20,287.91, asilimia
18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 27,457.62 na tiketi sh.
89,916.
Kamati ya Ligi sh. 6,762.63, Mfuko
wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,057.58, Chama cha Mpira wa
Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,703.05, gharama za mchezo sh.
6,762.63 na uwanja sh. 6,762.63.
Post a Comment