“Navishukuru sana vyombo vya
habari kwa kazi nzuri za uhamasishaji wa watu kushiriki katika Sensa ya
watu na Makazi japo vipo vichache sana vinavyoendesha mijadala ya
kuipinga”
Amesema maandalizi ya zoezi hilo
kwa mkoa wa Dar es salaam yamekamilika licha ya kuwepo kwa malalamiko
na madai ya baadhi ya makarani wachache kutolipwa fedha za mafunzo jambo
ambalo amesema mamlaka husika zinalifanyia kazi kwa kuhakikisha kuwa
ukamilishaji wauhakiki na uthibitisho wa majina yao unakamilika leo.
“Kwa
upande wa jiji la Dar es salaam wengi wameshalipwa fedha zao na kwa
wale wachache ambao madai yao yanashughulikiwa nawahakikishia kuwa
watalipwa kwa kuwa fedha yao ipo” amesisitiza.
* KUHUSU MADALE
Serikali imesema kuwa
haitayavumilia makundi ya watu wanaovunja sheria za nchi kwa kuendesha
vitendo vya wizi, uvunjaji wa nyumba, uporaji na uuzaji wa ardhi kinyume
cha sheria katika maeneo yanayomilikiwa kihalali jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Bw. Saidi Meck Sadiki ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam
kufuatia vurugu zilizotokea katika eneo la Madale nje kidogo ya jiji la
Dar es salaam kutokana na uamuzi wa serikali kuwaondoa kwa nguvu
wananchi waliovamia maeneo hilo.
Amesema kuwa serikali
haikukurupuka kuchukua hatua hiyo na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa
zimezingatia kanuni na taratibu za kisheria zikiwemo baraka za kamati
ya ulinzi na usalama ya mkoa.
“ Kufanyika kwa zoezi hili si
kwamba serikali ya Kinondoni imekurupuka, hata kidogo haijafanya hivyo,
zoezi hili limefuata kanuni na taratibu zote za kisheria ikiwemo uamuzi
wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es salaam na amri ya
Mahakama”
Amefafanua kuwa matukio
yaliyotokea hivi karibuni katika maeneo hayo kwa baadhi ya makundi ya
wananchi hasa vijana waliobeba silaha za jadi kuwashambulia, kuwajeruhi
na kuharibu mali za wananchi wanaoishi katika eneo la Madale kihalali
kwa lengo la kuwaondoa kwa nguvu na kuyatwaa maeneo yao ni jambo
lisilokubalika nchini.
Amesema kuwa licha ya jambo
hilo kuwa la muda mrefu na serikali kuchukua hatua za kuhakikisha kuwa
wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kihalali wanafanya shughuli zao
bila kusumbuliwa baadhi ya wananchi wamekuwa hawakubaliani na jambo hilo
na hatimaye kuanza kuyavamia maeneo ya wazi ambayo mengine yanamilikiwa
na taasisi na makampuni.
Ameongeza kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo hayo lilizingatia taratibu zote ikiwemo hatua ya serikali kuwapa taarifa wahusika wote waliovamia maeneo hayo kuondoka wenyewe jambo ambalo hawakulifanya.
“Kabla ya kutumia nguvu kuwaondoa wananchi hao serikali
iliwapatia taarifa ya kuwataka kuondoka wenyewe jambo ambalo walilikaidi
na kuendelea kukalia maeneo hayo kinyume cha sheria.Ameongeza kuwa zoezi hilo la kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo hayo lilizingatia taratibu zote ikiwemo hatua ya serikali kuwapa taarifa wahusika wote waliovamia maeneo hayo kuondoka wenyewe jambo ambalo hawakulifanya.
“ Bado naendelea kusisitiza kuwa serikali ilifuata taratibu zote, kwanza tuliwashauri wamiliki halali kwenda mahakamani kisha mahakama ikatoa amri ya wavamizi hao kuondolewa na zaidi ya hapo walipewa taarifa ya kuondoka wao wenyewe jambo ambalo hawakulifanya na hii inaashria kudharau amri ya mahakama” amesisitiza Bw. Sadiki.
Aidha Bw. Saidi Meck Sadiki amesema kuwa imebainika kuwa baadhi ya wananchi wanaoendesha vitendo hivyo vya kihalifu sio raia wa Tanzania na kukongeza kuwa tayari vyombo vya dola vinavyohusika vinaendelea na uchunguzi wa suala hilo na tayari vinawashikilia watu 68 kwa kuhusika na vurugu hizo.
Pia ameonyeshwa kusikitishwa na baadhi ya watendaji wachache wa serikali na viongozi wa siasa wanaoshabikia na kuhamasisha suala hilo na kuongeza kuwa serikali inaendelea na uchunguzi wa suala hilo na ikibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Post a Comment