waziri Mbarawa akitoa hutoba.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte akitoa mada katika mkutano wa capacity Africa.
naibu waziri, january Makamba na Mkurugenzi Mkuu wa Six Telecoms, Rashid Shame akiwa na Mkuu wa kampuni ya Main One Cable Fun
======== ======== ========
Na Mwandishi wetu.
Serikali
imesema itatumia shs 30 bilioni kukamilisha ujenzi wa mkongo wa taifa
na kurahisisha huduma hiyo hapa nchini. Hayo yalisemwa na Waziri wa
mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi
wa mkutano wa sita wa wadau wa mawasiliano duniani (Capacity Africa)
uliodhaminiwa na kampuni ya Six Telecoms ambao umefanyika Tanzania kwa
mara ya kwanza kwa siku mbili.
Mbarawa
alisema ujenzi huo huko kwenye awamu ya pili huku km 7560 zikiwa
zimemalizika kuunganishwa na tayari zimeanza kutumika kwenye makao makuu
ya mikoa yote nchini na tayari kampuni sita kutoka Rwanda, mbili za
Malawi, mbili za Zambia na mbili za Burundi zimeomba kuunganishwa
kwenye mkongo wa taifa," alisema Mbarawa katika mkutano huo. Mkutano huo
uliondaliwa na kampuni ya Six Telecoms umewakutanisha wadau wa
mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia kuitumia
Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika.
Mkurugenzi
mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema ujio wa mkongo
wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwenye sekta
hiyo. Shamte alisema lengo la mkutano huo ni kuitumia Tanzania kuwa
njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na kuongeza kwamba
hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya
mawasiliano hapa nchini.
Alisema
kuwa wamefarika sana kufanikisha mkutano huo na kutambulisha mtandao
wao wa Metro ambao unaongoza katika soko kwa hivi sasa. Kwa mujibu wa
Shamte, pamoja na changamoto kadhaa wanazokabiliana nazo, wameweza
kujidhatiti ili kuweza kufikia lengo lao hapa nchini na katika makampuni
mengine nje ya Tanzania yanayotumia huduma yao.
“Ninafuraha
kubwa kuona mkutano huu wa Capacity Africa unafanyika hapa nchini na
mwitikio kuwa mkubwa, kwa kweli hii ni faraja sana kwetu, najua mkutano
huu utatoa picha ya nini kitafanyika ili kukabiliana na changamoto
ambazo watumiaji wa huduma zetu wanakabiliana nazo, naipongeza serikali
kwa kutoa sapoti kubwa na wadau wote duniani kukutana na hili ni kwa
ajili ya kujenga na kuleta maendeleo katika nchi zetu,” alisema Shamte.
Wadau
wa mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia
kuitumia Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika.
Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja
Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo. Alisema kuwa lengo la mkutano huo
ni kuitumia Tanzania kuwa njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana
nazo na kuongeza kwamba hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa
watumiaji wa sekta ya mawasiliano hapa nchini.
Wadau
wengine waliodhulia mkutano huo ni wawakilishi kutokaLiquid Telecom,
WIOCC, Safaricom Business, Seacom, Gateway na kampuni mbalimbali za
mawasiliano duniani.
Post a Comment