Viongozi
wa nchi za Sudan kaskazini na Sudan Kusini wamefikia makubaliano yenye
vipengele tisa kuhusu baadhi ya tofauti zao, lakini wameshindwa kumaliza
mzozo juu ya jimbo la Abyei na suala la ukomo wa mipaka ya mataifa yao.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amesema kuwa nchi hizo zitasaini “Itifaki ya Uhusiano” leo hii.
Msemaji
wa Sudan Kusini Atif Kiir amesema kuwa Rais Omar Hassan al-Bashir wa
Sudan na rais Kiir wamekubaliana juu ya masuala ya kiuchumi na kuundwa
kwa ukanda maalumu usioruhusu shughuli za kijeshi katika eneo la mpaka
baina ya mataifa hayo.
Ameongeza kuwa hatua hiyo ni ili kuruhusu shughuli za usafirishaji mafuta.
Kiir
amesema kuwa usafirishaji wa mafuta ambao Sudan iliusitisha mapema mwaka
huu, utarejea tena na kwamba ni masuala ya kiufundi tu ndiyo
yaliyosalia kuanza upya kwa zoezi hilo.


Post a Comment