Katibu
Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, Nevile Meena akihutubia katika
mkutano uliofanyika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam jana, kulaani
ktendo cha Polisi kumuua kwa bomu Mwandishi wa habari wa Kituoc ha
Televisheni cha Channel Ten, Mkoa wa Iringa, marehemu Daudi Mwangosi
katika vurumai zilizotokea wakati Chadema wakifungua tawi katika Kijiji
cha Nyololo, wilayani Mufindi hivi karibuni.
Meena
akihutubia huku anionesha vidole vitatu akiiambia Serikali kuwa Vyombo
vya Habari hata bila kuandamana vinaweza kuitikisa nchi hata kwa
kutangaza kwamba wanahabari hawataweza kwenda kuripoti mikutano ya
hadhara ya vyama vya siasa kwa kutangaza kuwa ni maeneo hatari.
Maandamano hayo yalianzia Channel Ten hadi kwenye viwanja hivyo.Awali
walitakiwa kufanyika mkutano viwanja vya Mnazi Mmoja lakini uongozi wa
Manispaa ya Ilala, uliwakatalia. PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
Wanahabari wakiwa na huzuni huku mmoja wao akiwa na bango lenye ujumbe wa kulihoji jeshi la Polisi
Mmoja
wa wanahabari akiwa ameziba mdomo wakati wa mkutano huo. Hiyo ni
ishara kwamba kutokana na kifo cha mwandishi mwenzao,. Serikali inapanga
kuwaziba midomo wanahabari nchini
Wanahabari wakichangia ubani kwa ajili ya rambirambi ya familia ya Mwangosi Mohja ya mabango yenye ujumbe Mhadhili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Azavery Gwaitama akitoa mtazamo wake Mwandishi Mkongwe, Mas akipaza sauti yake. Wanahabari wakiwa na picha ya marehemu, Daudi Mwangosi Polisi wakilinda doria kwenye mkutano huo.

Post a Comment