Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki(kulia)
akipokea msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio
nchini Uingereza kuwasaidia wakazi wa Mabwepande walioathiriwa na
mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba 2011 jijini Dar es salaam leo.
Wanaokabidhi msaada huo ni kutoka kushoto ni Awadh Salim mkurugenzi wa
Kampuni hiyo, Bw. Mohammed Abdulrahaman Meneja wa kampuni hiyo Tanzania
na Bw. Chris Lukosi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya
Serengeti.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd) Bw. Chris Lukosi akimkabidhi Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki(kulia)
moja ya boksi lenye vitu mbalimbali vilivyotolewa na watanzania waishio
nchini Uingereza kuwasaidia wakazi wa Mabwepande walioathiriwa na
mafuriko yaliyotokea mwezi Desemba 2011 jijini Dar es salaam.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam akiwaeleza jambo viongozi wa Kampuni ya
Usafirishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight Forwarders Ltd)
iliyosafirisha bure msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo viatu, nguo na
vifaa vya watoto vilivyotolewa na watanzania waishio nchini Uingereza
kuwasaidia wakazi wa mabwepande.
Viongozi
wa kampuni ya ya Usafrishaji wa Mizigo ya Serengeti (Serengeti Freight
Forwarders Ltd) Bw. Chris Lukosi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia) mara
baada ya kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na
watanzania waishio nchini Uingereza leo jijini Dar es salaam.
Picha na Aron msigwa – MAELEZO
on Tuesday, September 25, 2012
Post a Comment