Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha
lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya
Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni
mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani
nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya
Kajima.
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na balozi wa
Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na
viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa
inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA ya Japan kutokana
na barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na
serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa
gharama zake.
Wafanyakazi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa leo jijini Dar es salaam
Waziri
wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni
akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF),
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia)
Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo
jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya
China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na
linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015
Loading...
Post a Comment