Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Serikali ya Japani yatia sahihi mikataba ya kusaidia Ujenzi wa Mabweni 4 wilaiani Nachingwea na Ruangwa Mkoani Lindi Msaada Unaogharimu USD 243.6


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea,Arbogast Kiwale kwa pamoja na Balozi wa Japan
Nchini Tanzania ,Masaki Okada wakitia saini mkataba wa kusaidia Ujenzi wa Mabweni mawili ya shule ya sekondari ya kutwa ya wasichana Nachingwea wenye thamani ya dola za marekani 122,333...Mkataba huo
umesainiwa mbele ya Wabunge wa mkoa wa Lindi,Wakuu wa wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri huku Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Katibu Tawala mkoa akishuhudia
Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkowe wilayani Ruangwa mwl Shannel Nchimbi akikabidhi hati ya makubaliano ya msaada wa mabweni 2 kwa shule hiyo kwa Balozi wa Japan,Masaki Okada hii katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Wabunge wa Mkoa wa Lindi nao wakishuhudia kuwekwa kwa saini mikataba ya Kusaidia ujenzi wa Mabweni 2 ya shule ya sekondari ya Nkowe wilayani Ruangwa Pamoja na Mabweni mawili ya Shule ya kutwa ya wasichana Nachingwea
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Lindi wakishuhudia tukio hilo la msaada wa kuinua kiwango cha elimu
Picha ya pamoja baada ya kusainiwa mikataba hiyo. Serikali ya Japan imetoa Jumla ya dola za kimarekani 243,698 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa mabweni 4 kwa shule za sekondari za Nkowe wilayani Ruangwa Na Shule ya kutwa ya Wasichana wilayani Nachingwea Hatua hiyo imekuja katika jitihada za Nchi ya Japan kukuza Ushirikiano na Tanzania Balozi wa Japan Nchini Masaki Okada amelala wiAlayani Ruangwa Mkoani Lindi ambapo leo atatembelea shule ya sekondari NKOWE na Baadae kuelekea Wilayani Nachingwea. Picha na Habari toka kwa Mdau Abdulaziz video rec,Ruangwa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top