Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

1800 WAPOTEZA MAISHA KWA AJALI

JUMLA ya Watanzania 1,800 wamepoteza maisha katika ajali mbalimbali zilizotokea nchini kati ya Januari na Juni mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima, alipokuwa akikabidhiwa stika za Wiki ya Nenda kwa Usalama zilizotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Kampuni ya mafuta ya Puma.
Alisema katika katika kipindi hicho zilitokea ajali 11,163 ambazo mbali na kusababisha vifo hivyo, pia zimesababisha watu 9,000 kupata ulemavu wa kudumu.
“Kulingana na takwimu hizo, maana yake ni kwamba kila siku watu 10 wanapoteza maisha kwa ajali. Hatuwezi kuruhusu hali hii iendelee.
“Nawashukuru wadhamini kwa kampeni ya Wiki ya Nenda kwa Usalama mwaka huu Kampuni ya Airtel na Puma kwa kutoa mchango wao pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi Usalama Barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani,” alisema.
Pamoja na hilo, aliwahimiza watu wanaomiliki vyombo vya moto kwenda kukaguliwa ndani ya wiki hiyo na kwamba wasiofanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, alisema katika wiki ya maadhimisho hayo watatoa mafunzo maalumu kwa waendesha pikipiki, kwani ajali nyingi zinazotokea zinahusu vyombo hivyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano, alisema kampuni hiyo inajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya Watanzania na mali zao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Puma, Maregesi Manyama, alisema moja ya malengo ya kampuni hiyo ni usalama kazini kwa kutopata ajali, hivyo mchango wao huo utafanikiwa ikiwa utafanikisha kuepusha kifo hata kimoja.

CHANZO: Tanzania Daima
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top