“Kwanza kabisa tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa
makundi yafuatayo kutokana na kazi kubwa waliyofanya ya kutusaidia,kutupa moyo wakati tukukiwa katika wakati mgumu:
1. Viongozi wote wa klabu 14 na ushirikiano wao katika kutupa moyo wakati wa mapambano. Kitendo hicho kimeonyesha umoja
tulionao na kukomaa katika uongozi wa soka nchini.
Ushirikiano huo umetuwezesha kupambana vilivyo katika kusaka
maslahi ya timu pamoja na kusonga mbele katika suala udhamini pamoja
na Vodacom kushindwa kufuatwa matakwa yetu. Hali hiyo inatupa
moyo kuwa tunaweza kufanikia hapo baadaye.
Pamoja na TFF kushindwa kutoa msaada kwetu, klabu ziliweza
kupambana vilivyo na kuweka mkazo mkubwa katika ligi.
2. Shukrani zetu za pili kwa vyombo vya habari na wachambuz mbali mbali wa mpira wa miguu. Vyombo vya habari vimeweza
kufuatilia suala hilo kwa umakini mkubwa huku vikiuliza maswali ya
msingi na kuonyesha jinsi gani TFF imekukuwa ikipotosha suala hili.
3. Pia tunaweza kutoa shukrani kubwa kwa mashabiki wa soka
kwa kuonyesha sapiti kubwa na kuonyesha jinsi gani mpo bega kwa
bega na klabu mbali ya kuupenda mchezo wa soka na maendeleo ya mchezo
huo kwa
ujumla.
4. Shukrani zetu pia kwa Mdhamini wetu mkuu, Kampuni ya simu
ya mkononi ya Zante kwa kuonyesha kuwa ni mdau wa kweli kwa
asilimia 100 kwa kuonyesha nia ya dhati ya kuendeleza soka la vijana
pamoja na vipingamizi mbali mbali, hata hivyo hawakukata tamaa na kuheshimu mkataba wetu.
5. Mashabiki na wadau wa African Lyon na uongozi. Tunawapa shukrani kubwa kwa kuwa karibu nasi kwa kutupa moyo wakati wa mtafaruku mkubwa na kutuhamasisha katika mapambano haya.
Busara zao
zilituwezesha kufikia hatua hii ya leo.
Ndugu waandishi wa habari; Wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na
harakati za kuhakikisha kuwa kipngele cha Upekee katika udhamini
“exclusivity” kichoibuka kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Tupo mbele yenu kuweka kila kitu kuhusiana na suala hilo wazi
na katika mstari kutokana na sababu suala hilo limepotoshwa na
kuweka mtazamo hasi kwa klabu ya African Lyon.
Lengo letu la kwanza katika mkutano huu ni kusafisha jina la
African Lyon na hasa kutokana na mtazamo wa wengi kuwa tatizo hilo
limetokana na msimamo wa klabu yetu.
Ni jambo la kusikitisha na kutisha kuona kwamba chombo
kilichopewa mamlaka makubwa ya kuendeleza mpira wa miguu nchini
kuisukumizia lawama klabu ndogo kama wakati chanzo cha matatizo hayo
yanetokana na utendaji wao.
Kama hatutaweza kutatua tatizo hili kwa sasa, hatutaweza
kufikia muafaka hapo baadaye na linaweza kuzihusisha klabu kubwa na
mapambano yatakuwa makubwa zaidi.
Yafuatayo ni vithibitisho au “fact” ambazo tunawaomba kutoa
majibu:
1. Mkataba kati ya TFF na Vodacom Tanzania ulisainiwa Agosti
11, siku 4 kabla ya ligi kuanza
2. Klabu hazikuwa na taarifa kuwa mkataba umesainiwa na TFF panoja na ligi kuanza.
3. Klabu zilisisitiza kuwa mkataba unatakiwa kusainiwa
angalau kuwahusisha wajumbe watatu kutoka vilabu vya ligi kuu, jambo
ambalo halikufanyika.
4. Taarifa iliyotolewa na Rais wa TFF kuhusiana na kipengele
cha Upekee “exclusivity” na kuwapa sapoti Vodacom ilikuwa na
upotoshaji kwani kuondolewa kwa kipengele hicho si mara ya kwanza katika
soka la
Afrika na Dunia kw ujumla. Mfano: Ligi ya Ghana inadhaminiwa
na kampuni ya simu ya Glo Mobile Ghana amabpo timu ya Asante
Kotoko inadhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya MTN Ghana.
Huu
ni mfano mmoja kwani kuna mifano mingi tu.
5. Vodacom haita ilipa fidia African Lyon kwa kufunjika kwa
mkataba wao na mdhamini kutokana na kipengele cha upekee.
6. TFF haitailipa fidia African Lyon kwa kukubali kipengele
hicho katika hatua za mwisho kabla ya ligi kuanza.
7. Access to the contract for clubs to understand the clauses
and issues involved is limited to going to TFF office and looking
at the contract there.
8. Hakuna hata klabu moja inayofahamu kuhusiana na mkataba wa sasa ambao TFF inadai kuwa umepata Baraka zote kutoka kwa
viongozi wa klabu za ligi kuu.
9. Mkataba ambao umesainiwa hivi karibuni unawapa nafasi
Vodacom haki ya kukataa mapendekezo ya vilabu vya ligi kuu na
kuzifanya klabu hizo kuwa katika wakati mgumu wa kupata mdhamini mwingine.
10. Fedha za udhamini zitolewazo na Vodacom hazitoshi
kuendesha klabu kutokana na urefu wa lligi na masuala mingine.
African Lyon haiwezi kupingana na Vodacom kwa sababu mkataba ulisainiwa baina yao na TFF. Hata hivyo kisheria tuna kesi
ngumu sana na TFF na tunapenda kuuliza maswali haya mawili na kupata
majibu yake.
1. Wanatarajia klabu kuweka nguvu zao pembeni za kupata
mdhamini mwingine mpaka TFF isaini mkataba na Vodacom ambao ulisainiwa
siku nne kabla ya ligi kuanza?
2. Je mnaweza kuishusha daraja African Lyon kama itashindwa kwenda kucheza mechi za ligi mkaoni Kagera au Mbeya kutokana
na kukosa fedha?
Instead of TFF making a case to the public that they
unsuccessfully worked with clubs to try and remove the “exclusivity” clause,
they are the ones making a case on behalf of Vodacom’s marketing
department that the “exclusivity” clause should have been there.
Why
would you fight Vodacom’s battle with the public who clearly feel that
the “clause” hurts the development of this game?
African Lyon inataka yafuatayo kutoka kwa TFF:
1. TFF lazima ikubali kuwa mtatizo haya ya mkataba
yamesabaishwa na wao kutokana na kushindwa kufuata utaratibu uiowekwa na
klabu na kusainiwa wao mkataba
2. TFF ikubali kuwa itaendeleza mkataba mpya wenye mabadiliko baada ya kumalizika kwa huu.
3. TFF ikutane na Zantel na kuwashukuru kwa kutojitoa katika majukumu yake na African Lyon,”
Sherally
Abdallah
Msemaji
African Lyon
Post a Comment