Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Airtlel,
Beatrice Singano Malya akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari, pamoja nae ni
Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor
Mkurugenzi wa Airtel Sam
Elangalloor, (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Makao
Makuu ya Ofisi z Airtel Morroco jijini Dar es Salaam leo wakati wakitangaza
promosheni mpya ya “Jipatie Mara 5” kwa wateja wake wan chi nzima. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Airtlel, Beatrice Singano Malya na
kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Cheikh Sarr.
Dar es salaam Octoba 2012
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe
itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama
“Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO ya wastani wa
matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.
Akiongea wakati wa uzinduzi
wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Airtel
tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi nzima mara tano ya wastani wa kiwango
cha pesa watakayotumia kila siku promosheni hii ya “Jipatie Mara
5”.
Promosheni hii itawazawadia
wateja wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi
itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo , hii
ni sawa na asilimia 500 ya bonus.
”Tumefanya hivi ili
kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha dhamira yetu
ya kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea aliongeza Elangalloor
.”
Akifafanua juu ya
promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano
Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari ameshaunganishwa katika promosheni
hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa
matumizi yako ya siku kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo
anajipatia nafasi zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa
maongezi
“Jipatie Mara 5” ni
promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila mteja atapata ujumbe
utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha kupokea ujumbe mara atakapopokea
asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa maelezo zaidi juu ya huduma hii piga
0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma
zetu”aliongeza Mallya.
Airtel inaendelea kuboresha
huduma za mawasiliano nchini. kwa kupitia huduma ya Airtel money, Airtel
imewawezesha watanzania kupata huduma za kifedha kirahisi katika maeneo
mbalimbali nchini.
Kwa kuthibitisha uwezeshaji
wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha wateja wake kutuma na
kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila makato yoyote. Vile vile
Airtel imeendelea kupanua zaidi huduma za internet kwa kuwezesha miji zaidi ya
30 nchini kupata internet yenye kasi ya 3.75G .




Post a Comment