Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ANTONY DIALO AMBWAGA CLEMENT MABINA, MWANZA


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina akimwaga sera zake jukwaani mbele ya Wajumbe (hawapo pichani) huku Wagombea wengineo nao pia wakimsikiliza kwa umakini mkubwa kabla ya kufia jukwaani (kura kutokutosha) ambapo Anthony Dialo alimwacha mbali kwa kura

Wajumbe kutoka Ukerewe.



Wajumbe kutoka Nyamagana.


Wajumbe kutoka Sengerema.

Wajumbe kutoka Kwimba.


Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi mkoa wa Mwanza mbunge wa Sengerema Mh. William Ngereja akitoa maelezo juu ya taratibu mbalimbali za mchakatomzima unaoendelea uwanjani hapa akiwa meza kuu na Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na Uratibu wa Bunge Mh. William Lukuvi (katikati) na katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Joyce Masunga.

Mwenyekiti wa CCM wilaya Geita Joseph Kashegu aka Musukuma (kushoto) na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani Shanslaus Mabula.

WajumbezZZZ mkutanoni ....

 

Pichani Wadau wa uchaguzi wa mkutano mkuu wa mkoa wa mwanza wakijipanga kabla ya uchaguzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa CCM Kirumba jijini Mwanza.


Wajumbe kupitia utaratibu uliowekwa walijipanga kwenye mistari kwenda kupiga kura kuchagua viongozi nafasi mbalimbali.


Huu ndio utaratibu wa zoezi la kupiga kura katika Mkutano mkuu wa mkoa wa Mwanza.




Kisha unatumbukiza hapa kwenye vyombo hivi vya wazi...


Zoezi gumu la uhesabu kura ukafuata....


Wajumbe wakaserebuka kusubiri matokeo ingawa simu zilizuiwa kuingia kwenye chumba cha kuhesabu kura.. lakini wapi...!! Habari zilipenya, mara tetesi kwa upande wa magharibi wakiwa wamenuna kumaanisha kuwa imekula kwao, nao mashariki wakifunguka kwa matabasamu kumaanisha yaliyomo yamo, ukiuliza aku tunafurahia muziki...tehe-te..




Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (kura 4), Hussein Mashimba (kura15), Joseph Langula Yared (kura 30), na Mabina ambaye alipata (kura 328) wote kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa

 
Wakati wa kutoa shukurani mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti hicho na kuangushwa Mh. Clement Mabina mbali na kupinga matokeo hayo waziwazi akidai kuwa atakwenda kukata rufaa, ilidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ambapo mmoja wa wagombea alidaiwa kutoa rushwa ya sh. 50,000 kwa kila mjumbe, kati ya wajumbe wanaokadiriwa kufikia 988, na kwamba inadaiwa kigogo huyo alitumia zaidi ya sh. Milioni 56 kwa lengo la kutafuta ushindi wa nafasi uenyekiti.
Maneno hayo yaliifanya meza kuu kuwa na tafakuri za kina huku minong'ono ya hapa na pale ikitawala... sssssSSSSSsssss!!!...
 

Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi alisimama na kusema kuwa mkutano huo ni halali na umefuata taratibu zote hivyo kama Mabina anadai kuwa si halali kwa vigezo alivyotaja basi akate rufaa na tume ya uchunguzi haito bagua kukagua mgombea anayelalamikiwa tu! bali itakaguwa wagombea wote wa nafasi ya U-enyekiti mkoa.

Diallo akitoa neno la shukurani...
 
 
 
 
 
 




Mwenyekiti mpya Dr. Anthony Diallo akizungumza na waandishi wa habari.

Anthony Mwandu Diallo; Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Mwanza
                                          *****************************
WAZIRI wa zamani wa Maliasili na Utalii, na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Anthony Mwandu Diallo, ameibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kisha kumgalagaza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Clement Gregory Mabina.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye uwanja wa mpira wa CCM Kirumba jijini hapa, ulionekana kuwashangaza baadhi ya wajumbe kutokana na kitendo cha baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka katika shule ya Sekondari ya Bwiru ya Wasichana, kuachishwa masomo yao kisha kupewa jukumu la kuhesabu kura za wagombea.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wana CCM na wananchi wa kawaida waliohudhuria uchaguzi huo, walisikika wakilalamikia kitendo cha wanafunzi hao waliokuwa wamevalia sare za shule hiyo, kuachishwa masomo yao shuleni kisha kupewa kazi hiyo ya kisiasa ya kuhesabu kura.
Mbali na hilo, ilidaiwa kuwepo kwa mchezo mchafu ambapo mmoja wa wagombea alidaiwa kutoa rushwa ya sh. 50,000 kwa kila mjumbe, kati ya wajumbe wanaokadiriwa kufikia 988, na kwamba inadaiwa kigogo huyo alitumia zaidi ya sh. Milioni 56 kwa lengo la kutafuta ushindi wa nafasi mojawapo zilizokuwa zikiwaniwa.
Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (4), Hussein Mashimba (15), Joseph Langula Yared (30), na Mabina ambaye alipata kura 328 kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa.
Awali, wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi walijikuta wakilipuka kumshangilia kwa nguvu kubwa aliyekuwa Waziri wa Naishati na Madini na mbunge wa jimbo la Sengerema, William Ngeleja, baada ya jina lake kutajwa kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo.
Uchaguzi huo ulifanikiwa pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza, ambapo waliochaguliwa na wilaya wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Mwamba Makune na Christine Mwalu Jilala (Misungwi), Joseph Langula Yared na Marco Mabihya (Sengerema), Stella Aya, Raban Mageje (Magu).
Wengine ni Angelina Mabula, Dede Swila (Ilemela), Sikitu Sanziyote na Charles Marwa Nyamasiriri (Nyamagana), George Nyamaha na Benadethar (Ukerewe), huku wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wilaya Kwimba waliochaguliwa ni Bujiku Philip Sakila na Dominic Kadaraja.
Uchaguzi huo ulifanikiwa pia kuwachagua wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza, ambapo waliochaguliwa na wilaya wanazotoka kwenye mabano kuwa ni Mwamba Makune na Christine Mwalu Jilala (Misungwi), Joseph Langula Yared na Marco Mabihya (Sengerema), Stella Aya, Raban Mageje (Magu).
Wengine ni Angelina Mabula, Dede Swila (Ilemela), Sikitu Sanziyote na Charles Marwa Nyamasiriri (Nyamagana), George Nyamaha na Benadethar (Ukerewe), huku wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Mwanza wilaya Kwimba waliochaguliwa ni Bujiku Philip Sakila na Dominic Kadaraja.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top