wadau wa elimu wilaya ya Kilolo wakiwa na mfanyabiashara Salim Asas |
KAMANDA wa umoja
wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Salim Abri Asas
ametoa msaada wa mifuko 200 ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi
milioni 3.2 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa mabweni ya wasichana katika
shule nne za sekondari wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Akikabidhi msaada
huo leo ofisini kwake Asas alisema kuwa amelazimika kuchangia ujenzi huo wa
mabweni ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali iliyopo madarakani chini
ya Rais Jakaya Kikwete ambapo suala la elimu limekuwa likipewa kipaumbele
zaidi.
Alisema kuwa mbali
ya kuchangia ujenzi huo katika wilaya ya Kilolo pia amepata kufanya hivyo
katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na maeneo mengine ya mkoa wa
Iringa.
Alisema kuwa
wilaya hiyo ya Kilolo kupitia mkuu wa wilaya Gerald Guninita waliandika barua
kwake kuomba kusaidiwa ujenzi wa shule za sekondari na mabweni katika wilaya
hiyo ya Kilolo.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita mbali ya kumpongeza Asas ambaye pia ni
mmoja kati ya wafanyabiashara mkoani Iringa bado aliomba wadau wengine wa
elimu katika mkoa wa Iringa wakiwemo wafanyabiashara kujitokeza kuchangia
maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo ya Kilolo.
Hata hivyo mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa saruji hiyo itagawanywa mifuko 50 kwa shule
nne za sekondari ambazo zinaendelea na ujenzi wa mabweni ya watoto wa
kike.
Alizitaja shule
za sekondari ambazo zitanufaika na msaada huo kuwa ni sekondari ya
Uhambingeto,Gangwa ,Ukwega na Masisiwe .
Aidha mkuu huyo
wa wilaya ametangaza kuwachukulia hatua kali wale wote wanaowapa mimba
wanafunzi na kuwa tayari ameagiza viongozi kuanza kuwasaka wahusika wa mimba
za wanafunzi ili kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
chanzo: Francis godwin
Post a Comment