Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

BAADA YA YANGA KUMSUSA, TOM SAINTFIET APATA ULAJI MWINGINE KWA MATAJIRI WA KIARABU

Mtakatifu Ton na Bin Zubeiry

Na Mahmoud Zubeiry
KIZURI chajiuza. Naam, habari ndiyo hiyo. Kocha Mbelgiji Tom Saintfiet aliyefukuzwa Yanga baada ya siku 80 za kuwa kazini, amepata mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Yemen kuanzia mwezi huu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Sana’a, Yemen mida hii, Mtakatifu Tom alisema kwamba anatarajia kuiongoza timu hiyo ya Magharibi mwa bara Asia katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Magharibi mwa Asia (kama Kombe la Challenge la CECAFA) itakayofanyika nchini Kuwait Desemba mwaka huu.
Alisema katika michuano hiyo, amepangwa kundi moja na Saudi Arabia, Iran na Bahrain na Januari mwakani, ataiongoza timu hiyo katika Kombe la Gulf huko Bahrain.
“Kwa sasa nipo katika Jiji la Sana'a na kesho nitaanza kazi kwa kambi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki Beirut, Oktoba 16 dhidi ya Lebanon,”alisema Mtakatifu Tom.
Saintfiet alifukuzwa Yanga baada ya kutofautiana misimamo na uongozi wa Yanga, akiwa amefanya kazi siku 80 na kuiachia timu taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Saintfiet amefungwa mechi mbili Yanga katika mechi 14 alizoiongoza timu hiyo tangu ajiunge nayo, Julai mwaka huu, akirithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar Papic.
Katika mechi hizo, zimo sita za Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, ambazo aliiwezesha Yanga kutwaa taji, ikipoteza mechi moja tu dhidi ya Atletico ya Burundi.
REKODI YA SAINTFIET YANGA
1.     Yanga Vs JKT Ruvu             (Kirafiki)               2-0
2.     Yanga Vs Atletico (Burundi, Kagame)                0-2
3.     Yanga Vs Waw Salam (Sudan, Kagame)            7-1
4.     Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)                    2-0
5.     Yanga Vs Mafunzo (Z’bar, Kagame)                  1-1 (5-3penalti)
6.     Yanga Vs APR (Rwanda, Kagame)                    1-0
7.     Yanga Vs Azam (Kagame)                                 2-0
8.     Yanga Vs African Lyon (Kirafiki)                       4-0
9.     Yanga Vs Rayon (Kirafiki, Rwanda)                   2-0
10.                        Yanga Vs Polisi (Kirafiiki, Rwanda)           2-1
11.                        Yanga Vs Coastal Union    (Kirafiki)          2-1
12.                        Yanga Vs Moro United      (Kirafiki)          4-0
13.                        Yanga Vs Prisons    (Ligi Kuu)                  0-0
14.                        Yanga Vs Mtibwa (Ligi Kuu)                     0-3
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top