KIUNGO Joey Barton ameshindikana na hawezekani popote!
Tayari ameingia kwenye kashfa nyingine ya mchezo usio wa kiungwana akiwa katika
klabu yake mpya, Marseille.
Kiungo huyo alijiunga na timu hiyo ya Ufaransa Agosti
baada ya kufungiwa mechi 12 akiwa anachezea Queens Park Rangers msimu
uliopita.
Lakini inaonekana Barton ameshindwa kubadilika kitabia
hata baada ya kuhamia timu ya Ligue 1, baada ya kumchapa kiatu mchezaji wa
Istre, Guy-Roland Niangbo.
Cheki Joey Barton
anavyomtandika kiatu mchezaji wa FC Istres, Guy-Roland Niangbo katika mechi ya
kirafiki
Hapa wanatenganishwa
Barton na Niangbo baada ya kutaka kugombana
Hii inaweza kumuweka pabaya Barton anayejaribu kutafuta
fitness ya kucheza mechi kabla ya kuanza kuichezea klabu hiyo kwenye
ligi.
Lakini tukio hilo linakuja siku kadhaa baada ya
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukwaruzana na kipa wa AEL Limassol,
Matias Degra katika Ligi ya Mabingwa.
Pia Barton haruhusiwi kucheza Ulaya, hadi Novemba 17
wakati Marseille itakapomenyana na Bordeaux.
Muingereza huyo alikiri hivi karibuni kwamba kadi
nyekundu aliyopewa katika mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England dhidi ya
Manchester City, Mei mwaka huu ilimuangusha sana.
Barton anampa mtu kitu
hapo..hebu cheki....
Barton aligombana na Carlos Tevez akapewa kadi nyekundu
baada ya kugombana na wachezaji wengine wa City, Sergio Aguero na Vincent
Kompany kabla ya kumvaa Mario Balotelli.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
Post a Comment