|
Picha zingine zinaonyesha jengo la kanisa hilo ambalo
limeteketezwa moto na watu wasiojulikana jana majira ya saa 4 usiku eneo la
Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji |
|
picha hizi zinaonyesha Mchungaji wa kanisa la
Pentecoste [MMPT] Emanueli Simoni [49] akiwa amesimama katikati akiwa ameshika
kenchi pamoja na waumini wenzake kwenye jengo la kanisa hilo lililoteketea kwa
moto na watu wasiojulikana jana majira ya saa 4 usiku eneo la Buronge katika
Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
|
************************Kanisa la Pentecoste [MMPT] lililopo Buronge katika
Manispaa ya Kigoma/Ujiji liisa hilo,mabechi 14, ubao wa kufundishia, mikeka 3
na mlango 1 viliteketea kwa moto. Jumla ya mali zilizoteketea kwa moto ni
Sh.Milioni 1,337,000. Kamanda huyo alisema “kiini cha tukio hili bado
kufahamika, hakuna madhara kwa binadamu, upelelezi wa tukio hili unaendelea ili
kuwabaini wahalifu hao kwa hatua za kisheria”alisema. Kwa upande wake
Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste [MMPT] Emanueli Simoni [49] alisema,”mimi
nilipata taarifa kuwa kanisa langu limeteketea kwa moto, nilikwenda polisi
Sentro kutoa taarifa, ndipo tulikwenda eneo la tukio tukakuta kanisa lote
limeteketea kwa moto”alisema. Eliasi alisema tukio hilo lilitokea jana majira
ya saa 4 usiku katika eneo la Buronge katika Manispaa ya
Kigoma/Ujiji. Alisema katika kanisa kulikuwa na Mabechi 14, Mlango 1, Vilago
3, Sanduku za kutozea sadaka na ubao wa kufundishia.Vyote vikiwa na thamani ya
Sh. Milioni 1,337,000 mali ya kanisa hilo. Alisema ajui watu waliochoma
kanisa hilo, wala hakuna mtu anayeshikiliwa na polisi kuhusiana na tukio
hilo. Mchungaji huyo anaiomba serikali iangalie sana matatizo ya uchomaji wa
makanisa sasa yanaenea nchi nzima. Pia amelitaka Jeshi la polisi Mkoani hapo
kufanya doria kwenye makanisa wakati wa usiku ili kukomesha vitendo vya uchomaji
wa makanisa. Alisema kanisa ni taasisi ya jamii hivyo anaomba serikali
ichangie gharama ya ujenzi wa jengo hilo ili wananchi wanaohabudu katika kanisa
hilo wapate sehemu ya kuabudia. Picha hii inaonyesha Mchungaji wa kanisa la
Pentecoste [MMPT] Emanueli Simoni [49] akiwa amesimama ameshika kechi kwenye
kanisa hilo lililoteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana majira ya saa 4 usiku
eneo la Buronge katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji. Picha hizi zinaonyesha
Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste [MMPT] Emanueli Simoni [49] katikati akiwa na
waumini wake wakiwa wamesimama kwenye jengo la kanisa hilo lililoteketea kwa
moto jana eneo la Buronge katika Manisipaa ya Kigoma/Ujiji na vitu vyenye
thamani ya Sh. Milioni 1,337,000 viliteketea kwa moto jana eneo la Buronge
katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji. |
|
on Wednesday, October 17, 2012
Post a Comment