Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiongozana na Balozi wa
Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi, wakati wakuingi a katika
ukumbi wa utamaduni wa Kihindi katika viwanja vya Bunge la India mjini
New Delhi.
Wakiwa
kwenye vazi maalumu waliloandaliwa, kutoka kulia ni Spika wa Bunge la
India na mwenyeji wa mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Mhe.
Meira Kumar, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na spika wa
Bunge la Swaziland Mhe Gelane T. Zwane.
Rais
wa Inter-Parliamentary Union (IPU), Bw. Abdelwahad Radi (wa pili
kushoto) na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders Johnsson ni miongoni mwa
viongozi mashuhuri waliohudhuria mkutano huo unaosisitiza wanawake
kupewa nafasi zaidi katika vyombo vya maamuzi.
Mapema
akihutubia mkutano huo Spika Makinda aliwaambia wajumbe kuwa wabunge
wanawake Tanzania ni 36% jambo ambalo lilifanya Tanzania kusifiwa na
kushauriwa kusonga mbele hadi 50%.
Picha ya pamoja ya baadhi ya maspika wanawake wa IPU ndani ya vazi maalumu waliloandaliwa.
Post a Comment