Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA DAR ES SALAAM CHAFANYIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akifungua kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dar es salaam leo. Pamoja na mambo mengine amewataka watendaji wa Halmashauri na Manispaa za jiji la Dar es salaam kusimamia kikamilifu matumizi sahihi ya barabara ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari jijini Dar es salaam. Wengine wanaoonekana ni Mhe. Idd Azzan(Mb) Makamu mwenyekiti wa Bodi ya Barabara mkoa wa Dar es salaam na Michael Mungaya kaimu (kulia) Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuph Mwenda akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili manispaa ya Kinondoni ikiwemo baadhi ya watu waliojenga maeneo yasiyoruhusiwa kutumia vibaya uhuru wa mahakama kufungua kesi na kukwamisha uendelezaji wa baadhi ya miradi ya barabara na ubomoaji wa baadhi ya nyumba zilizojengwa kinyumme cha utaratibu jijini Dar es salaam.
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) akichangia katika kikao cha Bodi ya Barabara ya mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa watendaji wa Halmashauri kusimamia ipasavyo makusanyo ya fedha ili kuziwezesha Halmashauri kuboresha miundombinu jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya  Temeke Bi. Magreth Nyalile akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na washiriki wa kikao hicho wakiwemo wabunge kuhusu hatua zinazochukuliwa na Halmashauri ya Temeke kujenga miundombinu na maegesho yatakayotumiwa  na malori yanayotoka bandarini na kupunguza  kero kwa watumiaji wengine wa barabara hizo kutokana na kushindwa kupitika kutokana na msongamano wa malori hayo.(PICHA NA ARON MSIGWA WA MAELEZO)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top