Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MPAKA CHUMBA CHA HABARI KINAHARIBIKA HIVI, TFF WANAPELEKA WAPI MAPATO YAO? AU HAWALIONI HILI?

Pichani ni sehemu ya paa la chumba cha habari cha chama cha mpira wa miguu Tanzania (TFF),ambacho kinatumika kukutana na Wanahabari wa vyombo mbalimbali  kuhusiana tasnia ya michezo kwa madhumuni ya kuihabarisha jamii.Kwa wanahabari za Michezo naamini kabisa mtakubaliana na mimi kuhusiana na hali iliyopo ndani ya ofisi hiyo,ambayo kimsingi nayo una umuhimu wake mkubwa,lakini imetelekezwa kama hivyo.
Chombo cha kutoa ubaridi ambacho kiliwekwa angalau kupunguza joto la Daslam ofisini humo,lakini kwa sasa ndege wamepata mahala pa kujipumzikia na kuzaliana,lakini sio ishu.
Taa nazo ziko hoi zinaning'inia tu,jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa watu.


Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo  mbalimbali wakisubiri wahusika wa TFF,kukutana na Wanahabari hao kwa ajili ya kuwapa taarifa mbalimbali za michezo,ili jamii ihabarishwe.
Dude la kuwekea Maji ya Kunywa ambalo sijui kwa mara ya mwisho  lilitumika lini,kwani limejaa vumbi,haliangaliwi tena.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top