CHAMA tawala cha Ukraine
leo kimedai kushinda katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana, huku matokeo ya
awali yakionyesha kinakabiliwa na ushindani kutoka kwa vyama pinzani vya Vitaly
Klitschko na Yulia Tymoshenko.
Waziri Mkuu wa Ukraine
Mykola Azarov ameelezea uhakika wake kwamba chama tawala kitashinda viti vingi
katika bunge jipya baada ya uchaguzi wa jana, ambao mataifa ya Magahribi yanaona
ni mtihani mkubwa kwa demokrasia ya Ukraine kutokana na kufungwa kwa mpinzani wa
Rais Victor Yanukovich.
Rais wa Ukraine Victor Yanukovich.
Hata hivyo chama cha bingwa
wa masumbwi Vitaly Klitschko kinaonekana kupoteza matarajio yake huku chama cha
mchezaji soka Andriy Shevchenko kikikuwa kinaonekana kushindwa vibaya katika
uchaguzi huo.
Chama cha Rais Yanukovich
kimepata asilimia 35.6 ya kura dhidi ya asilimia 21.5 ilizopata chama cha
upinzani cha Tymoshenko. Katika taarifa yake, tume ya uchaguzi imezingatia
asilimia 40 ya kura zilizopigwa kwa mfumo sawa wa kuamua viti nusu vya bunge
jipya.
Matokeo ya awali
yanaonyesha kuwa chama hicho tawala pia kilitarajiwa kushinda angalau viti 110
kati ya 225 vya bunge.
Akielezea kuhusu uchaguzi
huo Azarov amesema wanategemea kuwa chama tawala kitapata viti vingi katika
bunge jipya.
Aidha, chama cha
kikomunisti kilikuwa kimeshika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 15.1ya kura na
chama kipya cha UDAR kilichojitenga na Klitschko kikiwa kimepata asilimia
12.8.
Urusi na Umoja wa Ulaya
wanaufatilia uchaguzi huo.
Uchaguzi huo wa jana ni
mkubwa wa kwanza kufanyika nchini Ukraine ambao umeonyesha mvutano kati ya Umoja
wa Ulaya na Urusi tangu kiongozi aliyefanya mapinduzi ya chungwa mwaka 2004,
Tymoshenko kushindwa katika uchaguzi wa urais mwanzoni mwa mwaka 2010, uchaguzi
uliomuweka madarakani Yanukovich.
Urusi inaufatilia uchaguzi
huo kwa makini, huku Umoja wa Ulaya ukitaka viwango vya demokrasia vizingatiwe,
wakati ambao Ukraine inaendelea kusisitiza nia yake ya kujiunga na umoja
huo.
Waangalizi wa Shirika la
Usalama na Ushirikiano barani Ulaya-OSCE wanatarajia kutoa maamuzi yao kuhusu
uchaguzi huo baadae hii leo, ambayo yanafatiliwa kwa karibu kabisa kuona iwapo
kuna udanganyifu uliofanywa.
Viongozi wa Urusi na Umoja wa Ulaya.
Tymoshenko mwenye umri wa
miaka 51, alikamatwa Agosti mwaka uliopita wa 2011 na kuhukumiwa kifungo cha
mwaka mmoja jela baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya madaraka,
hukumu ambayo mataifa ya Magharibi na wafuasi wake wanaona kama ni njama za
kisiasa zinazofanywa Yanukovich.
Wasiwasi kuhusu utawala wa
miaka miwili wa Yanukovich ulioigawa Ukraine kutoka kwenye mkondo wake wa
demokrasia uliosababisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton na
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton kutoa wito wa
kufanyika uchaguzi utakaozingatia demokrasia
Post a Comment