WAKUU wa Sudan
wanasema watu kadha wamekufa kwenye shambulio lilofanywa na wapiganaji dhidi ya
wanajeshi wa serikali katika eneo la Darfur, magharibi mwa nchi.
Afisa mmoja wa
serikali alisema wanamgambo wanaounga mkono serikali wameuliwa katika shambulio
hilo la ghafla, karibu na al-Fasher, mji mkuu wa jimbo la North
Darfur.
Umoja wa
wapiganaji - Sudanese Revolutionary Front - ulisema ulifanya shambulio hilo na
kuuwa wanajeshi wa serikali na kuteka magari ya jeshi na silaha.
Baadhi ya makundi
ya wapiganaji ya Darfur mwaka jana yalitia saini mkataba wa amani na serikali ya
Sudan, lakini makundi mengine yanaendelea kupigana.
Post a Comment