Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Stephen Ulimboka, akisaini tamko lake kwa
watanzania ambalo lilisomwa kwa niaba yake na Wakili wake, Nyaronyo Kicheere,
Dar es Salaam. Kulia ni Wakili na Kamishna wa Viapo, Rugemeleza Nshala. Tamko
hilo alisaini Oktoba 07, jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyoimeeleza kuwa aliyekuwa
anawasiliana nae kabla ya kutekwa, kupigwa, kufungwa mikono na miguu,
kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa
Mabwepande usiku wa Juni 26 mwaka huu ni Bwana Ramadhani Ighondu ambaye alidaiwa
na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni Ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa
(TISS). Katika taarifa hiyo Dk. Ulimboka anaeleza kushangazwa na kutokamatwa mtu
huyo mpaka sasa na kudai kuwa yeye yupo tayari kutoa ushirikiano kwa tume huru
japo mpaka sasa haijaundwa.
Picha na Joseph
Senga
Post a Comment