Mtaalamu wa Elimu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF Zubeida Tumbo-Masabo
akitoa ufafanuzi kuhusiana na umuhimu wa kuwa na sera madhubuti za elimu
zitakazopelekea kuboresha kiwango cha elimu kuanzia ngazi za chini hadi za
juu.
Serikali ya Tanzania
imeshauriwa kuwa na sera ya mpya ya elimu kwa kuwa sera iliyopo imepitwa na
wakati na inasababisha mikanganyiko.
Mtaalamu wa Elimu wa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto –UNICEF Zubeida Tumbo-Masabo
amesema upo umuhimu wa kuharakisha kutoa sera mpya ya elimu kwa sababu ndio
itakayorahisisha utekelezaji badala ya kutokuwepo na sera inayo
eleweka.
Aidha amesema sera zilizopo
sasa zimepitwa na wakati, hivyo sera zitakazobuniwa upya zinapaswa kuwa na
malengo ya kuendeleza elimu kwa watoto haswa motto wa
kike.
Bi. Zubeida Tumbo-Masabo
amesema vitendo vinavyofanyika sasa vya kumfukuza shule mtoto wa kike kwa mfano
aliyebakwa na kupata ujauzito ni kumtia kitanzi cha
maisha.
Ametumia fursa hiyo
kuelezea kuwa katika sekta ya Elimu Umoja wa Mataifa unafanya shughuli za
kuboresha elimu kitaifa, lakini pia inafanya kazi katika ngazi ya wilaya maalum
katika kuangalia yale mambo ambayo wanayatilia mkazo na kuyachangia iwapo
yamefanikiwa.
Katika wilaya hizo Umoja wa
Mataifa unafanya vitu mbali mbali ambapo kama UNICEF imejikita katika kuangalia
Masuala ya Upangaji Mipango, kwa kuwa mara nyingi shule nyingi hazina
mipango.
Bi. Zubeida Tumbo-Masabo
amefafanua kuwa shule zinapokuwa na mipango thabiti zinaweza hata kuuza mipango
hiyo kwa mashirika mengine na kujipatia fedha za kuendesha shughuli zao nyingine
za hapo shuleni.
Post a Comment