Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba
vyombo vya ulinzi na usalama vimedhibiti hali ya ulinzi na imeimarishwa katika
maeneo yote ya Zanzibar.
Taarifa ya Serikali
iliyotolewa leo usiku na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,
Mohammed Aboud Mohammed ( pichani) amesema Zanzibar bado ni shwari na inaendelea
kuwa katika hali ya amani na utulivu.
Akizungumzia tukio la
vurugu zilizofanywa na wananchi wachache, Waziri Mohamed Aboud alisema vikundi
vya vijana vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vurugu
hizo katika mitaa ya Darajani, Michenzani, Muembeladu,Magomeni,Amani wakidai
Sheikh wao haonekani na kudhani amekamatwa na vyombo vya Dolan a kuwekwa
ndani.
Waziri Mohamed Aboud
alisema Serikali imewasiliana na vyombo vya Dola ikiwemo Polisi,Jeshi la
wananchi wa Tanzania, Idara ya Usalama wa Taifa, Vikosi vya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,KMKM,JKU,Chuo cha Mafunzo,Zimamoto na Valantia ambapo vyombo
vyote hivyo vimeeleza kutoelewa chochote kuhusu Sheikh
Farid.
Waziri huyo alisema kwamba
Jeshi la Polisi limepokea taarifa ya kutoonekana kwa Sheikh Farid ambapo kwa
sasa Jeshi hilo linaendelea kumtafuta na kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ili
kupata ukweli wake na kuchukua hatua zinazofaa.
Alisema kwamba wakati Jeshi
la Polisi likiendelea na upelelezi wake, wananchi wameombwa kutoa taarifa kuhusu
tukio hilo kwa vituo vya Polisi au kupitia Masheha, Ofisi za Wilaya na Mikoa
katika maeneo yao.
Waziri Mohamed Aboud
amesema Serikali inawasihi wwananchi waache kujiingiza katika vitendo vya fujo
na vurugu kwani kutenda hivyo ni kosa kwa mujibu wa sheria na Serikali
haitovumilia vitendo hivyo.
Katika tukio la leo mchana,
vijana hao wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Farid Hadi walifanya vitendo
vya vurugu ikiwemo kuchoma moto Maskazini za CCM,kuvunja maduka,kupora mali za
watu na kuharibu miundombinu ya barabara na kusababisha hasara
kubwa.
Post a Comment