Makamu wa Rais
SERIKALI imesema inaanza kuchukua hatua dhidi ya watu
wanaotumia
mwavuli wa dini kuleta vurugu
zinazotishia amani na usalama wa nchi.
Makamu wa rais Dk. Mohamed Gharib Billal,
amesema hayo leo wakati wa
kusherehekea sikukuu ya Eid el Hajji, ambayo
kitaifa imeathimishwa
wilyani Mwanga mkoani Kilimanjaro.
Akihutubia baraza la Eid, katika masjidi ya
Vuchama wilyani Mwanga,
Dk. Billal alisema hivi karibuni kumeibuka wimbi
la watu
wanaojihusisha na vurugu za kidini ambazo chanzo
chake kimekuwa ni
mgogoro miongoni mwa waumini wa
dini.
Dk. Billal alisema kwa kiasi kikubwa vurugu hizo
zimechafua sura y
taifa na kuleta taswira mbaya kwa jamii,
kutokana na uvunjifu wa amani
na sheria za nchi unaofanywa na kikundi cha watu
aliowaita wahuni.
Katika hatua nyingine Dk. Billal alisisitiza
umuhimu wa taasisi za
dini kujiendesha kwa misingi ya kushauriana na
kukubliana masuala
kadhaa ya kiutekelezaji na uendeshaji, ili
kuepuka mifrakano
inayojitokeza hivi sasa miongoni mwa pande
hizo.
Hata hivyo alisema serikali itaendelea kutimiza
wajibu wake wa
kuhakikisa kwamba amani inalindwa ili iweze
kuvisaidia vizazi vijavyo
na kuwa na nchi yenye uendelevu wa amani na
utulivu.
Naye kaimu mufti wa Tanzania sheikh Ismail Habib
Makusanya, wakati
akimkaribisha makamu wa rais kutoa hotuba yake
aliiomba serikali
kuharakisha utafiti na uchunguzi utakaowezesha
kubaini sababu za
kuvurugika kwa amani na utulivu
uliopo.
Alisema kwa kiasi kikubwa migogoro inayojitokeza
hivi sasa hususani
ile ya kidini ni tatizo linaloendelea kushika
kasi hali inayopelekea
kuwepo uhraka wa kulitatua.
“Amani inaletwa na watu wakiwemo viongozi wa
dini na serikali bila
kujali serikali hiyo ni ya Waislam au dini
nyingine na serikali hii
sasa inatambua kuwa wajibu wake kuhakikisha kuwa
amani inaendelea
kuwepo”, alisema.
Kaimu mufti alisisitiza serikali kutumia vyema
vyombo vyake vya ulinzi
na usalama kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya
wavunjifu wa amani
kwa haraka na kuchukua hatua zinazostahili kwa
wale watakaobainika
kuhusika.
Wakati huo huo ameelezea tishio la aadhi ya
wanasiasa wanaotumia
kivuli cha udini kuvuruga amani ya nchi na
kutaka nao wachunguzwe na
kuchukuliwa hatua za kisheria kama raia
wengine.
Sikukuu ya Eid el Hajji, imeambatana na uzinduzi
wa wa msikiti wa
Vuchama pamoja na kuweka jiwe la msingi na
uzinduzi wa mfuko wa
kujenga shule ya kituo cha Kiislam cha
Vuchama.
Miradi hiyo inatarajiwa kugharimu shilingi
bilioni 4.4, ambapo makamu
wa rais Dk. Billal alichangia shilingi milioni
tano, akifuatiwa na
viongozi wengine akiwemo waziri mkuu mstaafu
Cleopa Msuya, aliyetoa
shilingi milioni moja, huku mbunge wa Mwanga
Profesa Jumanne Maghembe
alichangia shilingi milioni
moja.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea salamu ya
heshma ya kikosi cha polisi FFU,alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani
Hotel,akiwa mgeni rasmi katika Baraza la EID EL HAJJ Leo.
********************
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed
Shein amesema kuwa Serikali kuanzia sasa itamshughulikia ipasavyo mtu yeyote
yule atakaye vunja amani ya nchi. Amesema kuwa Wamechoshwa na vitendo vya
uvunjivu wa amani Zanzibar hivyo Serikali haitomuonea huruma mtu yeyote
atakayediriki kuvunja amani kwani Serikali imesitahamili vya kutosha na sasa iwe
basi. Dkt Shein ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akihutubia Baraza la Idd-el-
Hajj lililofanyika katika ukumbi wa Salama, Hoteli ya Bwawani Mjini ZanzĂbar.
Amesema kuwa vitendo vilivyofanywa vinavyosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Jumuiya ya
UAMSHO vimesababisha mali za wananchi kuporwa,kuchomwa moto maskani za CCM
kuharibiwa kwa miundombinu ikiwemo barabara na hata kuuwawa kwa Koplo wa Polisi
kikosi cha FFU Said Abdulrahman. Amesisitiza kuwa Seikali itafanya kila
linalowezekana ili kuhakikisha kwamba wanaohatarisha Usalama na amani
wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria. Aidha Dkt. Shein amesema kuwa
zitatumiwa sheria na taratibu zilizopo ili kuvishughulikia vitendo vya uvunjifu
wa amani vitakavyofanywa au kuchochewa na kikundi chochote kile. Alisisitiza
kuwa hapana hata mtu mmoja aliye juu ya Sheria na kwamba kila mtu anapaswa
kufuata sheria . Rais Shein amesema kuwa hivi sasa hatua za kisheria zimeshaanza
kuchukuliwa,viongozi saba wa Jumuiya ya UAMSHO wameshapelekwa Mahakamani na
wengine waliokamatwa na Polisi kwa kufanya fujo nao pia wameshafikishwa
Mahakamani. Dkt Shein amewasihi wananchi wachache wenye nia ya kufanya fujo na
vurugu,waache kujiingiza kwenye vitendo hivyo kwani kufanya hivyo ni kufanya
kosa kwa mujibu wa sheria za nchi na seriakali haitowavumilia kwani ina wajibu
wa kusimamia sheria na kuwalinda wananchi. Alisema kuwa hivi sasa Jeshi la
Polisi na vyombo vya Ulinzi na usala vinaendelea na Doria katika mitaa mbali
mbali ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi kwa amani na utulivu.
Aliwahakikishia wananchi kuwa Mali zao na maisha yao yataendelea kulindwa,Wageni
wanahakikishiwa usalama wao na pia mazingira mazuri ya Utalii yataendelea
kuwepo. Dkt Shein aliwapongeza wananchi kwa uvumilivu na usatahamilivu kwa
kipindi chote cha vurugu na pia kuwa na subra ili kwa pamoja na Serikali
waendelee kushirikiana katika kuidumisha amani katika nchi. Alilipongeza Jeshi
la Polisi na vyombo vya ulinzi na Usalama kwa kazi nzuri wanayoifanya katika
kulinda amani ya nchi. Pia Dkt Shein alitoa mkono wa Pole kwa wananchi wote
waliopoteza mali zao au kupata athari za aina yoyote ile kutokana na fujo na
vurugu hizo zilizotokea .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 26/10/2012
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 26/10/2012
Post a Comment