Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akishiriki katika swala ya Iddi katika Masjid Rajab kijijini kwake
Msoga-Chalinze leo Asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete akipeana mkono wa Iddi na baadhi ya waumini walishiriki swala ya Iddi
katika Masjid Rajab Kijijini kwake Msoga, kata ya Chalinze,Wilayani Bagamoyo leo
asubuhi(picha na Freddy Maro)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la
Msikiti mpya wa Jihad, baada ya kuzindua rasmi Msikiti huo uliopo katika Kijiji
cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro, leo Oktoba 26, 2012 wakati wa
Sikukuu ya Eid El Hajj, iliyofanyika sambamba na uzinduzi wa Mfuko
wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari
ya Vuchama Mosque Islamic Centre.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini wa Dini ya Kiislam
katika Swala ya Idd El Hajj, iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad,
uliopo katika Kijiji cha Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada
hiyo ilifanyika sambamba na uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la
Msingi pamoja na uzinduzi wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa
Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre, leo
Oktoba 26, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa Swala ya Idd El Hajj,
iliyofanyika Kitaifa katika Msikiti mpya wa Jihad, uliopo katika Kijiji cha
Vuchama Wilaya ya Mwanga, Mkoa wa Kilimanjaro. Ibada hiyo ilifanyika sambamba na
uzinduzi wa Msikiti huo na uwekaji wa Jiwe la Msingi pamoja na uzinduzi
wa Mfuko wa uchangishaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Awali,
Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic
Centre,
leo Oktoba 26,
2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono
kuwaaga wananchi na waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka
eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na mmoja wa waumini
wa Kiislam wa Kijiji cha Vuchama wakati akiondoka eneo hilo baada
ya kuzindua na kuweka Jiwe la Msingi na kuchangisha fedha za ujenzi wa
Shule ya Awali, Msingi na Sekondari ya Vuchama Mosque Islamic Centre. leo Oktoba
26, 2012. Picha na OMR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa,baada ya kupokea salamu ya Hesha ya gwaride la Kikosi cha Polisi FFU,leo alipowasili katika viwanja vya Salama Bwawani Hotel, akiwa mgeni rasmi kulihutubia Baraza la EID EL HAJJ Leo.
Post a Comment