Francis Cheka |
BONDIA Francis Cheka ‘SMG’ anatarajiwa kupanda
ulingoni kuzipiga na Benjamin Simon wa Ujerumani Novemba 18, mwaka huu kwenye
ukumbi wa Universal, mjini Berlin nchini Ujerumani.
Awali mpambano huo ulikuwa ufanyike Novemba 17 mjini
humo, lakini umesogezwa mbele kwa siku moja na tayari Cheka amemwishashasaini
mkataba wa kukutana na mbabe huyo wa Ujerumani anayejulikana kwa jina la utani,
Iron Ben kutokana na ukali wa makonde yake.
Benjamin Simon |
Benjamin Simon amepigana mara 24 na kupoteza pambano
moja tu, wakati Cheka katika mapambano yake 33 amepoteza
sita.
Katika barua aliyomuandikia Eva Rolle wa kampuni ya
Prime Time Event Management ya Ujerumani, inayoandaa pambano hilo, Mwenyekiti wa
IBF/USBA, Lindsey Tucker alimfahamisha kuwa Rais wa IBF/USBA Daryl Peoples au
yeye mwenyewe, Lindsey Tucker watawasiliana na mama huyo kuhusu maofisa
watakaosimamia mpambano huo.
Hili litakuwa pambano la kwanza baina ya wababe hao,
wakiwaniataji la IBF la Mabara (IBF Inter Cintintal) na mpambano wao unategemnea
kutoa ushindani mkubwa.
Mshindi katika mpambano huo ataingia
moja kwa moja katika orodha ya mabondia 15 bora kwenye uzito wa Super Middle
duniani.
Post a Comment