ZAIDI ya Sh milioni 15 zinatarajiwa kutumika katika bonanza la michezo la wiki moja lililoanza jana, lenye lengo la kuimarisha michezo na mshikamano katika kata ya Kibada, Temeke mkoani Dar es Salaam.
Alisema matumizi ya fedha hizo yamegawanyika sehemu mbalimbali ikiwemo kununua seti za jezi, na mipira kwa ajili ya washiriki ambao ni kuanzia timu za watoto, vijana, wazee, waamuzi wa michezo hiyo na vyakula.
Akifafanua zaidi, Nkumbi alisema kuna vifaa vya wakina mama, ambao watashiriki katika mchezo wa kukuna nazi pamoja na zawadi zao.
“Hii michezo ina anza leo kwenye uwanja wa Shangwe kwa mtindo wa mtoano ambapo fainali za michezo yote zitafanyika Oktoba 31 mwaka huu huku tukimtarajia Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuwa Mgeni rasmi siku hiyo”alisema.
Aliitaja baadhi ya michezo itakayofanyika katika bonanza hilo kuwa ni pamoja na mpira wa miguu, netibali, Kuvuta kamba, kukimbia na gunia, drafti, bao, na riadha na mingineyo.
Nkumbi alisema kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa washindi pamoja na timu bora ambapo zawadi kubwa itakuwa fedha katika kila mchezo ambapo zawadi kubwa kabisa itakuwa sh 100,000
Post a Comment