Spika wa
Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na wasaidizi wake, akiwasili katika uwanja
wa ndege mjini Quebec, Canada Oktoba 20. 2012. tayari kwa kuhudhuria mkutano wa
127 wa chama cha Mabunge Duniani, (IPU), uliotarajia kufunguliwa rasmi leo
Jumapili Oktoba 21, 2012, na kumalizika Oktoba 26. Makinda ameongoza ujumbe wa
wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani
wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano
huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne
Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali ya mkutano na afisa kutoka
Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni
Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika
Mkutano huo nchini Canada.
|
Loading...
Post a Comment