Mshiriki wa Redd's Miss Tanzania 2012,Mary Chizi ndie alieibuka kidedea leo katika mashindano ya Michezo mbali mbali iliyowashirikisha warembo wote wa Redd's Miss Tanzania 2012,ambapo yeye ameweza kuwa kinara katika michezo mitatu mfululizoukiwemo wa kuogelea na kuwaacha wenzake wakijikongoja.Mary Chizi anaungana na wenzake wawili walioshinda mataji ya Miss Photogenic (Lucy Stephan) na Top Model (Magdalena Roy) ambao kwa pamoja wataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya Redd's Miss Tanzania 2012 mwaka huu.
Warembo walioingia hatua
ya Tano Bora katika mashindano ya Michezo Mbali mbali wakiwa kwenye picha ya
pamoja.
Warembo wa tatu
waliojihakikishia kuingia hatua ya nusu fainali ya Mashindano ya Redd's Miss
Tanzania 2012.Kutoka kulia ni Lucy Stephan (Redd's Miss Photogenic),Mary Chizi
(Redd's Miss Tanzania Sports Lady) pamoja na Magdalena Roy (Redd's Miss
Tanzania Top Model).
Mkurugenzi wa Kampuni ya
Lino Agency ambao ndio waandaaji Mashindani ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga
akitangaza mshindi wa jumla kwenye Michezo mbali mbali.
Bw. Yasson Mashaka
akitangaza washindi wa Michezo yote kabla ya kutangaza warembo walioingia hatua
ya tano bora.
Warembo wa Redd's Miss
Tanzania wakitoana jasho kwenye michezo mbalimbali hii leo Warembo wa Redds Miss
Tz wakishiriki kwenye mchezo wa wavu hii leo kwenye fukwe ya bahari ya hindi
kwenye mwendelezo wa maandalizi ya fainali ya Redds Miss Tz hapo mwezi ujao.
mbio za Magunia.
Mchezo wa Soka.
Mkuu wa Itifaki wa Kamati
ya Miss Tanzania,Albert Makoye akitoa maelekezo wa warembo wa Redd's Miss
Tanzania wakati wa kushindana kuruka umbali mrefu.
Mchezo wa
kuruka.
Mpira
wa Wavu.
Kuvuta
kamba.
Post a Comment