|
Waziri wa
Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe, (Kulia), akipokea ripoti ya uchunguzi wa
kashfa ya wizi na madudu mengine kwenye bandari ya Dar es Salaam, kutoka kwa
mwenyekiti wa kamati iliyochunguza "madudu" hayo, Bernard Mbakileki, ofisini kwa
waziri jijini Dar es Salaam Jumapili Oktoba 21, 2012. Kwa mujibu wa Mbakileki,
ripoti hiyo ya kurasa 285, imegundua mambo kadhaa :machafu" na imetoa
mapendekezo kadhaa ya hatua za kuchukuliwa ambapo waziri mwenye dhamana
amewaahidi watanzania kuwa taarifa ya hatua zitakazochukluliwa kufuatia ripoti
hiyo, zitatolewa Desemba mwaka huu wa 2012 ambapo amewataka Watanzania kuvuta
subira kwani kuanzia sasa, yeyote anayefanya kazi Bandarini, akithubutu kunyofoa
kitu basi nayeye atanyofolewa. Banadari ya Dar es Salaam, imekuwa kwenye shutuma
nyingi, ikiwemo kuchelewesha mizigo ya wateja, urasimu lakini baya zaidi wizi
uliokithiri wa mizigo ya wateja. Waziri Mwakyembe aliunda kamati hiyo kuchunguza
tuhuma hizo kufuatia hatua yake ya kumnsimamisha kazi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu
wa Bandari hiyo, Ephraem Mgawe na wasaidizi
wake |
|
Mwenyekiti
wa kamati iliyochunguza "madudu" kwenye bandari ya Dar es Salaam, Bernard
Mbakileki, akisoma ufupisho wa ripoti yao. |
on Sunday, October 21, 2012
Post a Comment