ULE uchumba uliodumu
kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba
‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na
kumvalisha pete ya uchumba.

H-Baba akimvisha pete ya uchumba, Flora
Mvungi.
Kinyume na ilivyozoeleka, zoezi la kutoa mahari kufanyika nyumbani, kwa wawili hawa ilikuwa tofauti kwani kila kitu kilimalizikia ukumbini humo.

H-Baba akiwasalimiana ndugu na
jamaa.

Flora Mvungi kabla ya kuvishwa pete ya
uchumba.
“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba na kuongeza:
“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”H-BABA
Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’, Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

Ndugu na jamaa waliohudhuria tukio
hilo.

H-Baba akiwasalimia wageni waalikwa.
chanzo: UjanaTz


Post a Comment