Loading...
HILI NDILO BONDE LA NGORONGORO
UKIBAHATIKA kutoka nje ya Tanzania unaweza kujitambulisha kwa nchi na kuitaja Ngorongoro, kwani ni rahisi kueleweka japo kuna alama nyingine kama Mlima Kilimanjaro na Mapango ya Amboni.
Wilaya ya Ngorongoro ni miongoni mwa maeneo yenye vivutio vya aina mbalimbali duniani.
Hii ni wilaya ambayo huwezi kulinganisha na wilaya nyingine hapa nchini kutokana na matukio yake.
Ngorongoro imebarikiwa kwa kiasi kikubwa kuwa na maajabu yaliyomo kwenye chati ya dunia.
Imekuwa ni kawaida kwa wageni kutoka nchi mbalimbali duniani wakija nchini kwa madhumuni ya kuona maajabu ya Bonde la Ngorongoro yaani Ngorongoro Kreta yenye wanyama wa aina mbalimbali hata wale ambao ni adimu kama vifaru.
Bonde hilo limekuwa ni kivutio kikubwa sana kwa wageni kutoka nje ya nchi hata kwa Watanzania wenyewe kwani maajabu yake ukiyatamka yanasisimua kwa historia yake inavyovutia.
Ngorongoro Kreta imekuwa ikiliingizia taifa letu fedha nyingi za kigeni kwa jinsi ilivyobarikiwa kuwa na matukio ya ajabu.
Kwani huko ndiko lilikogundulika fuvu la binadamu wa kwanza kwenye eneo linalotambulika kwa jina la Olduvai Gorge eneo ambalo pia limebeba umaarufu mkubwa duniani kwani watu wengi utembelea eneo hilo ili kujionea hali halisi.
Binadamu huyo aliyejulikana kwa jina la Zinjanthropus fuvu lake limesababisha kuwepo kwa makumbusho ambayo ni sehemu ya kivutio kingine kinacholingizia taifa fedha za kigeni na za hapa nchini.
Hilo ni tukio linaloiweka Ngorongoro kwenye wigo wa kutambulika kimataifa.
Umuhimu wa makumbusho hiyo umezidi kupanda siku hadi siku kwani hata hivi karibuni tulishuhudia maadhimisho ya miaka 50 ya makumbusho ya Olduvai Gorge na kuhudhuliwa na wageni na Watanzania waliyokwenda kushuhudia tukio hilo.
Wakati tukizungumzia hayo pia tunapaswa kufahamu kuwa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ndiyo hifadhi pekee inayojumulisha wanyama na binadamu kuishi kwa pamoja na kuwa marafiki.
Ukifika kwenye hifadhi hiyo hakika utastahajabu kwani wafugaji wa jamii za Kimasai wanajichanganya na wanyama kama mtu na jirani yake hakuna anayehofia mwenzake.
Ukitaka kufurahia maisha ya ukaribu wa wanyama na binadamu tembelea Hifadhi ya Ngorongoro.
BLOG RAFIKI
-
-
-
-
Kwa Undani4 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment