Mkurugenzi
wa Maisha Plus,Masoud Kipanya (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa
Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (pili kulia)
,Mwakilishi wa Idara ya Kilimo wa NMB, Carol Nyangaro (wa pili kushoto)
na Meneja wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB,Imani Kajula (kulia)
akiwagawia jarida la NMB Financial Fitness baadhi ya wakinamama wa Mama
Shujaa wa Chakula katika kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo
mengi yanayohusu uelewa wa matumizi ya fedha.
Mkuu
wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB ,Imani Kajula (kushoto)
akiwasomea jarida la NMB Financial Fitness wakinamama wa Mama Shujaa wa
Chakula katika Kambi ya Maisha Plus, jarida hilo lina maelezo mengi
yanayohusu matumizi mazuri ya fedha.
Meneja
wa Mikopo Midogo ya Biashara, Mashaga Changarawe.akipata kinywaji
kwenye kibuyu alipowatembelea wakinamama shujaa wa chakula katika kijiji
cha Maisha Plus.
**************
NMB ikiwa wadhamini wakuu wa
mpango wa mama shujaaa wa chakula, imewatembelea washiriki wa mama
shujaa wa chakula katika kijiji i cha Maisha Plus na kuwapa elimu ya
kifedha kupitia mpango wa NMB Financial Fitness.
NMB kupitia mpango wa NMB
Financial Fitness unaolenga kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya fedha
imepata fursa ya kuwaelimisha washiriki kuhusu huduma za kifedha,
uwekaji akiba, kupanga matumizi, matumizi mazuri ya kifedha na mengine
mengi.
Vilevile, Washiriki hao walielimishwa kuhusu Mikopo Midogo na kati ya kibiashara pamoja na mikopo ya kilimo. NMB inaamini udhamini huo ni
sahihi kutokana na kuwa utakuza kilimo na kuwasaidia wakulima wadogo
katika maisha, mapambano dhidi ya njaa,umasikini na uhaba wa ajira
miongoni mwa wanawake.
Post a Comment