Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

IBF NA OMAN ZAINGIA KWENYE HATUA ZA MWISHO KUHAMISHIA MAKAO MAKUU YAKE JIJINI MUSCAT


 
Nchi ya Oman kupitia kampuni ya Al Swayni Sports Services Ltd ya jiji la Muscat na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF zitaingia katika hatua ya mwisho tarehe 10 November 2012 y a majadiliano ya kuhamishia makao makuu ya IBF Africa, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Uajemi (IBF/AMEAPG) katika jiji la Muscat nchini Oman. Majadiliano haya yatafanyika katika jiji la Muscat, Oman.
Mazungumzo ya mwanzo yalianza mara tu baada ya mkutano wa 29 wa mwaka wa IBF uliofanyika katika jiji la Honolulu, Hawaii nchini Marekani mwezi wa sita ambapo programu “Utalii wa Michezo” iliwakilishwa na Rais wa IBF/AMEAPG Onesmo Ngowi wa Tanzania na kupitishwa.
Nchi ya Oman inataka kulitumia Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) lenye mtandao mkubwa zaidi ya nchi 200 duniani kujitangaza kibiashara kupittia “Utalii wa Michezo”
Matokeo yake baada ya kumalizika kwa makubaliano haya yanalenga kuundwa kwa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Ghuba ya Uarabu (IBF/AGBA).
Makubaliano haya yanaratibiwa na kaka wawili wakishirikiana na pamoja na serikali ya nchi ya Oman, Amin Saad Mabrook Bait-Saleem na Aymnan Saad Mabrook Bait-Saleem pamoja na Onesmo Alfred McBride Ngowi Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati, Ghuba ya Uarabu na Ghuba ya Uajemi (IBF/AMEAPG).
Akizungumza na kikundi cha waandishi maalum wa habari wa kimataifa, Rais wa IBF AMEAPG Onesmo Ngowi alisema kuhamia Oman ni mkakati wa uhamisho (Strategic Move) faida kwa IBF na nchi ya Oman kwa pamoja. Rais huyo alisema kuwa kwa sasa nchi nyingi duniani zinatafuta taasisi za kutumia kujitangaza na IBF ni moja ya taasisi zenye mtandao mkubwa duniani pamoja na kuheshimika sana.

Aidha, Oman inataka kutumia IBF kujenga uwezo wa kuwaandaa wanamichezo wa Oman watakaoshiriki katika mashindano yajayo ya Olimpiki ya Rio miaka mine kuanzia sasa!
Ngowi alisema kuwa kufanya shughuli za IBF kutokea Muscat, Oman kutasaidia kuwafikia watu wengi zaidi ya ilivyo sasa kwani serikali ya Oman kupitia Al Swayni Sports Services Ltd itawekeza katika kuijengea uwezo IBF kufanya sughuli zake kwa ufanisi zaidi.
Makubaliano haya yamewezesha kufanyika kwa mpambano wa kwanza wa ngumi wa kimataifa nchini Oman ambako bondia Francis Cheka atakutana na bondia maarufu wa Oman Amin aad Mabrook Bait-Saleem (DAGER) kugombea ubingwa ulio wazi wa “Ghuba ya Arabian” katika uzito wa Super Middle
Mpambano kati ya Amin Saad na Francis Cheka utakuwa ni wa utangulizi kwa mpambano kali kati ya bondia Vitali Klitshko kutoka Ukraine atakapopapmbana na bondia David Haye wa Uingereza katika mpambano uouopewa jina la “Mshikemshike katika Ghuba ya Arabia”
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top