Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
Inspekta Jenerali Saidi Mwema, amesema kuwa ili kuifanya nchi yetu
iendelee kuwa salama, kuna haja ya kuwekeza zaidi katika miundombinu ya
amani.
IGP Mwema ameyasama hayo leo
mjini Zanzibar wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya uongozi wa kati kwa
askari Polisi kwenye Chuo cha Taaluma ya Polisi mjini Zanzibar.
Amesema bado kuna haja ya kila mwananchi kuelewa kuwa jukumu la usalama wa nchi hii liko mikononi mwake.
Amesema kila mmoja hawezi kukwepa
jukumu la kulinda rasilimali yake na mfano mdogo ni pale kila mmoja kwa
wakati wake na bila ya kufundishwa pale anapolinda faragha.
IGP Mwema pia ameeleza umuhimu wa
kwa nini kila Mtanzania anapaswa kuwa mlinzi wa Taifa letu na kutilia
mfano kwamba suala la ufalama linaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja,
familia, kaya, kijiji, kata ama shehiya tarafa wilaya mkoa na Taifa.
Amesema katika taaluma ya Polisi,
Askari amefundishwa kuwa mlinzi katika mambo manne makubwa ambayo
yanamhusi kila mmoja wetu bila ya kujali nafasi yake katika jamii.
Mambo hayo ni manne ni fursa
ambazo zikiachwa wazi watu wengine wanachukua nafasi ya kuichukua nafasi
kuu nne ( four Speces ) sio kama askari lakini hatani kabla ya wa
mali wa mali zake, mlinzi wa familia wakiwemo watoto wake pamoja na
himaya inayomzunguuka.
Amewataka Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake, awe mdau wa sualama kama anavyolinda na kuheshimu faragha zake.
Kwa upande wake, Kamishna wa
Polisi Zanzibar CP Mussa Ali Mussa, amesema kuna haja ya kila kiongozi
wa Jeshi la Polisi hapa nchini kuyageuza matazo wanayowakabili kama
changamoto na kuzigeuza fursa ya kuleta ufanisi kazini.
Naye Mkuu wa mkoa wa Mjini
Magharibi Zanzibar Mh. Abdallah Mwinyi, ameelezea mikakati
inayochukuliwa na mkoa wake katika kudhibiti usalama wa maeneo
mbalimbali na kusema kuwa Ulinzi shirikishi na Polisi Jamii ni jicho la
Polisi mitaani.
Awali akitoa tathmini ya mafunzo
hayo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma za Polisi Zanzibat ACP Ramadhani Mungi,
amesema wahitimu hao wamejifunza mambo mbalimbali ukiwa ni pamoja na
kuimarisha ushirikiano kati ya Polisi na vyombo vya Habari.
Kamanda Mungi, amesema wameweka
somo hilo kwa kufahamu kuwa kazi za Polisi zinaingiliana kwa kiasi
kikubwa na zile za Waandishi wa Habari na kwamba kila mmoja anamtegemea
mwingine ili kufanikisha kazi zake.
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na
Mkuu wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Kamishna Khalifa Hassan Choum, Mkuu wa
Chuo cha Taaluma za Polisi Dar es Salaam ACP Ali Lugendo na Maafisa
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Vikosi vya SMZ.
Post a Comment