MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa ya Chama
cha Mapinduzi (CCM), Sophia Simba, amesema hamuogopi hata kidogo
mpinzani wake Anne Kilango, akitamba kuwa yeye ni mkimya.
Simba ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati akipongezwa na kushukuriwa na Shirikisho la Vyuo Vikuu Dar es Salaam kwa kuanza jumuiya hiyo vyuoni.
Akijibu maswali ya wanahabari waliotaka kujua ni nani anayemtisha katika mpambano huo, Simba alimtaja Mary Rose akisema kutokana na ujana wake na huenda akashangaza watu lakini akakataa kwa Kilango.
“Jamani mimi si mtu wa kupiga kelele, nadhani mnanijua mimi ni mtu wa kimya kimya si kama debe tupu ambalo haliishi kelele, mkitaka kujua haya ngojeni uchaguzi uishe tutajua tu,” alisema.
Simba aliongeza kuwa katika uongozi wake wa miaka minne amefanya mengi na kwamba anajivunia maendeleo ya kuwavuta wanachama wengi kuingia bungeni, kufanikisha kupata wanawake wengi makatibu wa CCM mkoa na kujenga jengo la UWT mkoa.
Hata hivyo alisema kuna propaganda nyingi zinaenezwa juu yake lakini hazina ukweli wowote kwa kuwa kila mtu ana mikakati yake katika kuhakikisha anashinda hivyo kuzuliwa mambo si ajabu.
Lakini pia alisema kuwa hata kama hakuchaguliwa kuendelea na nafasi hiyo ataendelea kuitumikia UWT kwa moyo wake wote kwa kuwa bado atakuwa ni mbunge pia.
Shirikisho hilo, likiongozwa na Mwenyekiti wake, Zelda Musa, lilisema kuwa linamshukuru Simba kwa kuwa yeye ndiye muanzilishi wa umoja huo vyuoni.
chanzo: Tanzania Daima

Post a Comment