
Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba, mgeni rasmi wa TWENDE 2011,
akiangalia bidhaa za ubunifu zilizotengenezwa na wajasiriamali wabunifu wa hapa
nchini katika Jukwaa la Wanawake
Wajasiriamali Tanzania- TWENDE, 2011 viwanja vya mnazi mmoja. Kulia ni meya wa Halmashauri
ya wilaya ya Ilala Mhe. Jerry Silaa pamoja na Musatafa Hassanali, mjasiriamali mbunifu na muasisi wa
TWENDE (kushoto).
1.
Mgeni rasmi wa TWENDE 2011,
Mh. Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bi. Sophia Simba
akishangazwa kwa umahiri na uzuri wa kazi za ubunifu za mmoja kati ya
wajasiriamali wanawake walioshiriki Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE,
2011 katika viwanja vya Mnazi Mmoja
jijini Dar es slaam. Pembeni yake kulia ni Mh. Jerry Silaa, meya wa Halmashauri
wa wilaya ya ilala, na kushoto ni Musatafa Hassanali, mjasiriamali mbunifu na
muasisi wa TWENDE.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dr. Cyril Chami
akipokea maelezo juu ya ubunifu uliotumika katika utengenezaji wa bidhaa ya
kiutamanaduni kutoka kwa mshiriki wa TWENDE, 2011 katika viwanja vya manazi moja
jijini Dar es salaam.
Washiriki wa TWENDE 2011, wakisalimiana na Waziri wa
Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami mara baada ya waziri huyo kuwatembelea
katika banda lao na kujionea bidhaa
wanazotengeneza.
----
·
TWENDE 2012 KUFANYIKA KWA
MWAKA WA TATU SASA
·
SEMINA NA MAONESHO YA
TWENDE NI KUANZIA TAREHE 18 HADI 20 YA MWEZI WA KUMI KATIKA VIWANJA VYA MNAZI
MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM.
·
WANAWAKE WAJASIRIAMALI
KUELIMIKA, KUUZA BIDHAA ZAO NA KUKUZA MTANDAO WA KIBIASHARA KUPITIA JUKWAA LA
WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA- TWENDE
Jukwaa la
Wanawake Wajasiriamali Tanzania- TWENDE linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 18
– 20 ya mwezi wa kumi 2012 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
TWENDE imekuwa ikifanyika kila mwaka kwa
mwaka watatu sasa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2010, lengo likiwa ni kuwaleta
pamoja wanawake wajasiriamali wadogo, wakubwa na wale wanaochipukia ili kupata
fursa ya kuuza, kuonesha na kujadili masuala ya biashara kwa
ujumla.
Sambamba na
hilo. TWENDE inalenga kusaidiana na serikali katika kutimiza malengo ya milenia
likiwemo
lengo namba moja ambalo linalenga kuondoa umasikini, namba tatu kutetea haki na
fursa sawa kwa wanawake, lengo namba tano kuhamasisha afya ya uzazi
na lengo namba nane, ambayo ni kuendeleza
uhusiano wa kudumu kwa ajili ya maendeleo ya jamii. Pia TWENDE inalenga Kukuza
uzalishaji kwa wanawake wafanyabiashara na kukuza mgawanyiko wa masoko sambamba
na muonekano wa wafanyabiashara wanawake katika
jamii.
Kwa upande wa mwaka huu TWENDE inatarajia kuwashirikisha wanawake
wajasiriamali wengi zaidi ambao wamekuwa wakifanya biashasha tofauti ili kuweza
kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi zaidi kibiashara.
Sambamba na semina bora zitakazotolewa kwa wanawake wote ambao watapata elimu
itakayotolewa wataalamu wa fani mbalimbali
Kwa miaka mitatu mfululizo TWENDE imekuwa ikitoa fursa kwa wanawake
wajasiriamali kukutana pamoja na kujadili mafanikio na changamoto ambazo
zimekuwa ni kikwazo cha wanawake wajasiriamali kutofikia malengo yao kibiashara.
“Licha ya kwamba wanawake wengi wamejikita katika sekta hii ya
ujasiriamali, lakini bado wamekuwa wakikabiliawa na changamoto mbalimbali
zinazokwamisha kufikia malengo yao, ikiwemo elimu ya ujasiriamli na upatikanaji
wa mikopo, kwa hiyo ipo haja kwa wanawake kujijengea utaratibu wa kushiriki
katika fursa kama hizi zinazowajengea uwezo”. Alisema Saphia Ngalapi Meneja
Mradi wa TWENDE.
Zaidi ya Wanawake Wajasiriamali Wanawake 100 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani wanatarajai kushiriki katika TWENDE mwaka
huu, ampabo maonesho hayo yanakwenda sambamba na semina zitakazo tolewa kwa
wanawake wote bure, kwa wale watakaoshiriki katika maonesho, na hata wale ambo
watakuwa hawakupata frusa ya kuonesha na kuuza bidhaa
zao.


Post a Comment