Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKUTANO MKUU 2012 WA WATANZANIA WAISHIO UJERUMANI WAFANA KWA KISHINDO FRANKFURT

Meza kuu katika mkutano wa Umoja wa watanzania Ujerumani

Kamanda Ras Makunja wa FFU (mwenye kofia) akiwa chini ya ulinzi


(Naibu Balozi Mh.Ali Siwa (mwenye suti nyeusi) akiwa na viongozi wa UTU)
****************************
Mkutano mkuu wa watanzania waishio ujerumani  uliofanyika siku ya jumaamosi tarehe 29. 09 2012 Mjini Frankfurt katika kitongoji cha Raunheim. ulifanikiwa kutimiza malengo yake na maazimio yake  Moja wapo ilikuwa ni kufanya uchaguzi wa uongozi wa umoja huo, kabla ya kufanyika uchaguzi huo na mjadala  wa maazimio ya umoja huo, Mgeni rasmi katika mkutano huo mwana diplomasia naibu balozi wa Tanzania nchini ujerumani mheshimiwa Bw. Ali Siwa alitoa nasaha zake na salamu kutoka Ubalozi wa Tanzania Nchini ujerumani kwa watanzania waliohudhuria katika mkutano huo, kwanza aliwapongeza watanzania kwa kufanikiwa kuunda umoja huo wa watanzania waishio ujerumani ambao ndio mwamvuli mkuu wa mshikamano wa watanzania wote nchini ujeruman, isitoshe Bw. Ali  Siwa aliwaambia watanzania kwamba ofisi yake ipo wazi wakati wowote iwapo umoja huo utahitaji ushauri wowote utakaoleta  maendeleo ya umoja huo na watanzania kwa ujumla, aliwaasa watanzania kuwa mshikamano wao na umoja wao ndio utakaokuwa ufunguo  na sauti ya maendeleo yao na vizazi vwao ugenini na nyumbani pia. baada ya nasaha hizo  wananchama wa umoja wa watanzania  walichagua viongozi wao kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti: Mfundo Peter Mfundo, Makamo: M/Mwenyekiti. George Mtalemwa. Katibu: Bi Tulalumba Mloge. Muweka hazina: Bi Mwamvua Dugala Merkel.

Umoja huo wa Watanzania Ujerumani (UTU) ndio chombo pekee kilichopata usajili kwenye serikali ya ujerumani, na kutambuliwa kisheria,  ambacho kinawaunganisha watanzania wote wanaoishi ujerumani, na ndio Daraja linalowaunganisha  watanzania waliopo Nyumbani na kwengineko ughaibuni. Kwa watanzania wanaopenda kujiunga na umoja wa watanzania ujerumani (UTU) milango ipo wazi,  wasiliana na  kamati.utu@googlemail.com
“ Tuungane sote ! Umoja na mshikamano ndio mwanangaza na msingi imara wa maendeleo unaoleta maana kamili ya maisha” UMOJA NI NGUVU
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top