JESHI la Wananchi Tanzania
(JWTZ), limesema litafanya zoezi la kulenga shabaha kwenye Kambi ya
Mloganzila mkoani Pwani, kwa muda wa siku tatu kuanzia leo.
Msemaji wa Jeshi hilo, Kanali,
Kapala Mgawe alisema zoezi hilo ni la kawaida na litakuwa halina madhara
kwa wananchi hivyo wawe watulivu.
Alisema zoezi hilo linaaza leo
na litamalizika siku ya Jumatano ambapo limewataka wananchi wanaoshi
karibu kutoikaribia kambi hiyo.
Naye Menyekiti wa kijiji
cha Mloganzila, Mohamed Kikonyo, alisema jeshi hilo limeamua kuandaa
mazingira mazuri ya matangazo kwa kupita barabarani na kipaza sauti
lengo likiwa ni kuwafahamisha wananchi kuhusuzoezi hilo.
“Wakazi wote wa mkoa wa Pwani na
wale wa Dar es Salaam ndiyo wanaoishi karibu na kambi hii hivyo kila
atakayesikia tangazo hili ajaribu kumfahamisha mwingine kuhusu zoezi
hili ilikuepuka usumbufu” alisema Kikonyo
Alisema hatarajii kusikia
wananchi kukimbia nyumba zao baada ya kusikia milipuko hiyo kutokana na
ukweli kwamba milipuko hiyo itakayosikika haitakuwa na madhara.
Kikonyo alitoa wito kwa wananchi
kutii sheria kwa kuacha kusogelea eneo hilo la jeshi kwani kwa kufanya
hivyo ni sawa na kuingilia kazi za watu.
Ni hivi karibuni Jeshi hilo,
katika kambi hiyo, lilifanya zoezi kama hilo huku kukiwa hakuna taarifa
zilizotolewa kabla kitendo kilicholeta usumbufu kwa wananchi kukimbia
makazi yao na kutokomea kusikojulikana hadi siku iliyofuatia.
Post a Comment