DIWANI wa Kata ya Saranga
(Chadema), wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ametoa siku saba kwa
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kutekeleza makubaliano ya mradi wa ujenzi
wa barabara ya Kimara hadi King’ongo kinyume chake wakazi wa eneo hilo
wataandamana.
Kauli hiyo imekuja baada ya
wakazi hao kuhoji kuhusu sh milioni 300 zilizotolewa na wafadhili wa
Japan, Mei mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa
kilometa 3.8, haujaanza hadi leo wakati fedha zipo.
Akizungumza na wandishi wa
habari jana jijini Dar es Salaam, diwani huyo, Efraim Kinyafu, alisema
wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitaabika kwa muda mrefu kutokana na
ubovu wa barabara hiyo kitendo kwamisha shughu zao za maendeleo.
Alisema wameamua kutumia
utaratibu huo wa kuandamana kama njia sahihi ya kufikisha kilio chao kwa
wafadhili waliojitolea fedha hizo, hata hivyo, itategemea iwapo siku
saba zitapita bila ya mkandarasi kuwepo katika maeneo hayo
Kinyafu alisema wafadhili hao
walipinga fedha hizo kupitia kwenye Akauti ya Manispaa ambapo
walikubaliana zipitie kwenye Akauti ya kata.
Akifafanua zaidi, alisema baada
ya makubaliano hayo ofisi ya kata iliwasilisha Akaunti yake kwa
Mkurugezi kisha utekelezaji wauingizaji wa fedha hizo ulikamilika tangu
Mei mwaka huu.
“Unajua wananchi hawaelewi kuna
nini kinaendelea wakati kuna jumla y sh milioni 350 amapo kati ya hizo
halmashauri imechangia milioni 50 isitoshe hata kapuni ya ujenzi ya
COSCO imeishapewa tenda ya kazi hiyo”alisema kinyafu.
Kinyafu alitoa angalizo kwa viongozi wa Manispaa hiyo kuepuka mgogoro huo kwani unaweza ukawa mkubwa zaidi kushinda ule ulijitokeza wakati wa sensa ya makazi na watu kutokana na ukweli kwamba waathirika safari hii ni wengi.
Alisema mvutano huo wa
ucheleweshwaji wa miradi mingi katika maeneo yanayoongozwa na vyama vya
upinzani kunachangiwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wakidhani kuwa
kukamilika kwa miradi hiyo kwa asilimia 100 kutawajengea umaaruf
wapinzani hao, kuwafanya waendelee kuchaguliwa katika chaguzi nyingne
kitendo ambacho hakina uhakika.
Post a Comment