KIUNGO wa Manchester United, Shinji Kagawa anakabiliwa na maumivu ya goti, ambayo yatamuweka nje ya Uwanja kwa wiki tatu hadi nne.
Kocha wa United, Sir Alex Ferguson amethibitisha habari
hizo katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo.
"Kagawa atakuwa nje kwa wiki tatu hadi nne kutokana na
maumivu ya goti. Aliumia katika mechi na Braga Jumanne katika Ligi ya
Mabingwa,"alisema Mscotland huyo.
Post a Comment