Waumini
wakihuzunika baada ya shambulio.
**********************
UMOJA wa Mataifa
kupitia ofisi yake ya usaidizi nchini Afghanistan, UNAMA, imelaani vikali
shambulio la leo kwenye msikiti mmoja huko Maimana katika jimbo la Faryab nchini
humo lililosababisha vifo vya 40 na wengine 56 wamejeruhiwa.
Mwakilishi maalum
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchiniAfghanistan, Ján Kubiš, amesema
shambuliohilolimetokea wakati wa sala ya Eid el Adha ambapo mtu aliyekuwa
amevalia fulana yenye mabomu alijilipua wakati akiingia kwenye msikiti wa Eid
Gah mjini humo.
Amesema
shambuliohilobaya zaidi kwenye msikiti lililosababisha vifo vya raia
waAfghanistanhalina uhalali wowote na linapaswa kushutumiwa na watu wote kwa
nguvu zote.
Mwakilishi huyo
amesema wahusika wanawajibika kwa vifo vilivyotokea kutokana na
shambuliohilodhidi ya msikiti ambao kwa mujib uwa sheria za kimataifa za haki za
binadamu haipaswi kushambuliwa kwa kuwa ni sehemu za ibada.
Kutokana na
shambuliohilo UNAMA imetuma rambirambi zake kwa wafiwa na kuwatakia uponaji wa
haraka majeruhiwa wote.
Post a Comment