Kell Brook ametimiza
ndoto zake za kuwania ubingwa wa dunia, baada ya jana usiku kumtwanga
Muargentina Hector Saldivia katika raundi ya tatu kwenye ukumbi wa Motorpoint
Arena mjin Sheffield.
Bondia huyo Muingereza
mwenye umri wa miaka 26, alionekana kumzidi mpinzani wake kuanzia kengele ya
kwanza katika pambano lake la mwisho la mchujo kabla ya kuwania taji la IBF,
uzito wa Welter ambalo anapenda kuligombea mapema mwakani.
Brook aliahidi
kumtandika Saldivia ili kuilipia timu ya taifa ya soka ya England kisasi cha bao
la Mkono wa Mungu la Maradona.
Kell Brook kulia
akizipiga na Hector Saldivia
Brook akimpa kitu
Saldivia
Brook amemkalisha chini
Saldivia
Brook amemmaliza
Saldivia kwa kumkalisha chini
Brook akishuhudia
mpinzania wake akihesabiwa na refa Howard Foster
Brook akishangilia na
mwalimu wake
Sasa ni mshindani Namba
1: Brook akishangilia na promota wake Eddie Hearn
Post a Comment