MJUMBE wa amani wa kimataifa nchini Syria Lakhdar
Brahimi Jumamosi amesisitiza mjini Damascus haja ya kusitisha mapigano, ili
kuzuwia umwagikaji zaidi wa damu nchini nchini humo.
Brahimi alikutana
na waziri wa mambo ya kigeni Walid Muallem pamoja na viongozi wa upinzani
wanaokubalika na rais Bashar al-Assad , katika juhudi za kupata kuungwa mkono
mpango wake wa kupatikana usitishaji wa mapigano , wakati wa sikukuu muhimu ya
Kiislamu wiki ijayo.
Lakini mazungumzo
hayo yaligubikwa na hali ya wasi wasi katika nchi jirani ya Lebanon , ambako
viongozi wa upinzani pamoja na waziri mkuu walihusisha shambulio lililosababisha
mauaji ya afisa wa ngazi ya juu wa upelelezi na utawala wa Syria .
Mjumbe wa kimataifa Lakhdar
Brahimi.
Nchini Syria
kiasi watu 108 wameuwawa katika ghasia siku ya Jumamosi , 42 kati yao ni raia,
limeripoti shirika la kuangalia haki za binadamu nchini humo, wakati mapigano
yakiendelea katika maeneo ya kaskazini na kuzunguka mji wa
Damascus.
Kusitisha
mapigano.
Wizara ya mambo
ya kigeni imesema waziri Muallem amejadili pamoja na Brahimi, kile walichokiita
"hatua ya kusitisha mapigano, ili kujitayarisha kwa mjadala wa dunia juu ya
Syria, bila kuingiliwa na ushawishi wa mataifa ya nje".
"Mjadala wa aina
hiyo ndio njia pekee ya kutoka katika mzozo huo", wizara hiyo
imesema.
Muallem pia
amelalamika kwa Brahimi juu ya mataifa ya eneo hilo ambayo Syria inayashutumu
kwa kuwahifadhi, kuwapa silaha na kuwapa mafunzo waasi, akisema kuwa vitendo
vyao vinaathiri ujumbe wa mjumbe huyo wa amani wa umoja wa mataifa ya mataifa ya
Kiarabu, Arab League.
Uturuki
na Saudia zalaumiwa.
Syria imeilaumu
mara kwa mara nchi jirani ya Uturuki pamoja na nchi yenye utajiri mkubwa wa
mafuta ya Saudi Arabia na Qatar kwa kuunga mkono wapiganaji waasi.
Brahimi ana
matumaini ya kupata usitishaji wa mapigano wakati wa sikukuu ya Waislamu ya Eid
al-Adha, inayoanza Oktoba 26, akiamini kuwa hiyo inaweza kusafisha njia ya hatua
za muda mrefu za amani.
Hassan Abdel Azim
kutoka taasisi ya uratibu wa kitaifa kwa ajili ya mabadiliko ya kidemokrasia
nchini Syria , kundi la upinzani linalovumiliwa na utawala wa nchi hiyo ,
ameunga mkono pendekezo hilo la kusitisha mapigano.
Kiongozi wa upinzani nchini Syria Hassan
Abdel-Azim.
Usitishaji kama
huo wa mapigano unaweza kusafisha njia kwa ajili ya hatua za kisiasa , iwapo
utapanuliwa kujumuisha kuachiwa huru kwa wafungwa ambao wamekamatwa na utawala
wa nchi hiyo pamoja na usambazaji wa msaada wa madawa kwa raia walioathirika,
amesema.
"Ghasia nchini
Syria zimefikia katika kiwango cha kutisha ambacho kinatishia usalama na uhuru
nchi hiyo", Abdel Azim ameongeza baada ya kukutana na Brahimi.
Nayo
makundi ya upinzani
Ukichukua msimamo
mkali zaidi , makundi ya upinzani ambayo yako nje ya nchi hiyo yanasema utawala
wa Syria ni lazima uchukue hatua ya mwanzo na kusitisha mashambulio yake ya kila
siku.
Brahimi
anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Assad baadaye leo (21.10.2012) katika juhudi
za ujumbe wake mjini Damascus kuleta amani.
Mjumbe huyo
amefanya ziara katika mataifa kadha ambayo yana ushawishi katika mzozo huu wa
Syria katika muda wa wiki moja iliyopita, ikiwa ni pamoja na ziara nchini
Lebanon na Iran, na kuonya kuwa ghasia zinaweza kusambaa na kuliwasha moto
katika eneo lote.
Post a Comment