Victoire
Ingabire.
**********
KIONGOZI wa upinzani
nchini Rwanda Victoire Ingabire amehukumiwa miaka minane gerezani baada ya
kupatikana na hatia ya kosa la uhaini.
Viongozi wa mashtaka
walitaka afungwe maisha jela kwa kutishia usalama wa nchi.
Mahakama imempata na
hatia ya kupuuza mauaji ya Kimbari yaliyotokea mwaka 1994.
Ingabire hakuwa
mahakamani wakati hukumu ilipotolewa dhidi yake kwani amekuwa akisusia
kuhudhuria vikao vya kusikilizwa kwa kesi hiyo akisema imeshinikizwa
kisiasa.
Alikamatwa mwezi Aprili
mwaka 2010 na kuzuiwa kushiriki uchaguzi uliofanyika mwaka huo
Post a Comment