Kocha
wa ngumi za kulipwa Christopher Mzazi, kutoka Gym ya "No Ttalking" ya Mabibo ya
jijini Dar es Salaam, ameamua kuwapoza machungu mabondia chipukizi, Mwaite Juma
na Baina Mazola, waliowahi kupiganishwa na Promota, Kaike na kisha kuwadhurumu
malipo yao ya pambano hilo.
Mabondia
hao wanatarajia kupanda Ulingoni Novemba 18/2012 huko maeneo ya Mabibo katika
ukumbi wa D.I.D, ambapo pambano hilo litakuwa ni la upinzani kubwa kutoka na
mabondia hao kutambia na kufikia kutaka kuzichapa kavu kavu
mtaani.
Akilizungumzia
pambano hilo kocha mzazi alisema kuwa mabondia hao wote ni wazuri ambao
wanaofundishwa na kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa pia ni mabondia wazuri na ni
tegemeo zuri la baadae.
''Sielewi
ni kwanini Kaike aliamua kuwafanyia uhuni na kuwadhurumu, hivyo mimi nikiwa kama
mzazi kama jina langu nimeona ni vyema nikawapoza machungu kwa kuwapa pambano na
mabondia wangu na kuwalipa zaidi ya pesa
walizodhurumiwa kwa kuwa ninaelewa machungu na ugumu wa mchezo wenyewe ulivyo''.
alisema mzazi.
Hivyo
basi Mwaite Juma, kutoka BigRight boxing gym atacheza na Baina Mazola wa No
talking gym katika pambano la raundi
nane.
Na
Pambano hilo kali litasindikizwa na Karim Ramadhan (mdogo wa Nasibu
Ramadhan-bondia bora wa mwaka) atakaecheza na Martin
Richard.
Siku
hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi ya kiushindani ya kuwekana sawa nani zaidi
ya mwingine kati ya mabondia wa mabibo na
mwananyamala.
Post a Comment