Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga kulia
akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuanza kuuzwa kwa tiketi za shindano
la Taifa la Redds Miss Tz kushoto kwake ni katibu mkuu wa kamati ya Miss Tz
Bosco majaliwa.
*******************
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi
wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim Lundenga amesema
kuwa,Kutokana na ukubwa wa shindano kwa mwaka huu wale wote
watakaofanikiwa kuingia ukumbini watakaa katika viti maalum vilivyowekwa
katika hadhi ya kimataifa na kila tiketi itagarimu kiasi cha shilingi
laki moja (100,000) za kitanzania.
Kwa
upande wa burudani kutakuwa na burudani nyingi sana na zitaongozwa nawasanii
nguli hapa nchini kama Diamond Platnum,Winfrida Josephat’Rachel’s pamoja na Wanne star ngoma
troupe.
Post a Comment